Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WANAHABARI IRINGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA HABARI KWA USAFI ,WAOMBA BUNGE KUONYESHWA LIVE

Wanahabari  mkoa  wa  Iringa wakishiriki  kufanya  usafi katika soko la Manispaa ya  Iringa  leo Mwenyekiti  wa matukio na maafa  ...


Wanahabari  mkoa  wa  Iringa wakishiriki  kufanya  usafi katika soko la Manispaa ya  Iringa  leo
Mwenyekiti  wa matukio na maafa  wa chama  cha  waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin (mwenye ndoo) akimwaga takataka katika dampo baada ya  kuzizoa ndani ya  soko kuu la Iringa  wakati wa shughuli za usafi  leo

Na MatukiodaimaBlog

WAKATI  leo  ni maadhimisho ya  siku  ya uhuru  wa  vyombo  vya habari duniani kwa  maadhimisho hayo  kitaifa  kufanyika mkoani Mwanza ,wanahabari  mkoa  wa Iringa  kuitumia siku hiyo   kufanya usafi  wa mazingira  katika  eneo la soko  kuu la Manispaa ya Iringa.

Huku wakiomba serikali kuangalia upya uamuzi wake wa kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni kuwa ni kuwakosesha wananchi kupata uhuru wao wa kupata habari.

" Huo ni uhuru wa kuzaliwa nao.sheria zote zinazotungwa zinapaswa kuzingatia haki hiyo. Miaka 15 iliyopita tz ilikuwa na sheria 16 zinazominya uhuru wa habari, hivi sasa sheria hizo zimeongezeka hadi 26 na serikali iko mbioni kupeleka nyingine hivi karibuni. .....Wanahabari na wadau wake tukikubali serikali iendelee kutuletea sheria za aina hiyo tutakawa tunakubali kujenga ukuta wa kuzuia Upatikanaji na usambazaji wa habari. ...tunaomba serikali izingatie maoni ya wadau wakati ikitunga sheria hizo"

Mwenyekiti  wa kamati ya matukio na maafa  wa chama  cha  waandishi wa habari  mkoa  wa Iringa (IPC) Bw  Francis Godwin  alisema  kuwa  shughuli   hiyo  inatarajiwa  kuanza majira ya  saa 2.30  asubuhi   hii kwa  wanahabari  wote  mjini  Iringa  kushiriki usafi kabla ya  kuendelea na majukumu  yao ya  kila  siku.

Alisema imekuwa ni  kawaida  ya  wanahabari  mkoa  wa Iringa  kufanya maadhimisho hayo kwa aina  tofauti  tofauti  ikiwemo ya kusaidia  watu  wenye mazingira  magumu  ,kuchangia maendeleo ya  mkoa  huo upande wa  elimu na  kuwa mwaka jana  waliadhimisha   siku  hiyo kwa kutoa mifuko ya  saruji ya Tsh  500,000 kwa  mkuu  wa wilaya ya Iringa kwa ajili yakuchangia ujenzi wa maabara .

Hata  hivyo  alisema kwa  kuwa  wanahabari ni chachu  ya maendeleo katika  jamii  wataendelea kufanya shughuli mbali mbali za kijamii katika  mkoa wa Iringa na  kuiomba  jamii kujenga  utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo  yao.

Pia  alisema ni  vema  Manispaa ya  Iringa ama  serikali ya mkoa  kutunda  sheria kali itakayowabana  wananchi  wanaotupa taka  ovyo kwa  kuwatoza faini kati ya Tsh 50,000 ama 100,000 ili kukomesha tabia  hiyo.

Kwani  alisema upo uwezekano wa  kutoa ajira kwa  vijana kuzunguka mitaani kukamata  wanaochafua mazingira na  kuwapeleka ofisi za mwanasheria wa Manispaa na kuwatoza faini na kama faini ni Tsh 50,000 basi kijana atakayekamata mchafuzi wa mazingira alipwe Tsh 30,000

Alisema   kuwa kauli mbinu ya maadhimisho  hayo ya  siku ya  uhuru  wa  vyombo vya habari ni UPATIKANAJI  WA HABARI NI UHURU  WA KIMSINGI ,HIVYO  NI HAKI YAKO

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WANAHABARI IRINGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA HABARI KWA USAFI ,WAOMBA BUNGE KUONYESHWA LIVE
WANAHABARI IRINGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA HABARI KWA USAFI ,WAOMBA BUNGE KUONYESHWA LIVE
https://1.bp.blogspot.com/-DkbDppmsOK4/VyiDK864MBI/AAAAAAACHPs/X5ALH_ij9hQ8LsqFJ5UBFzkp-oyj9fmHgCLcB/s640/IMG-20160503-WA0143.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-DkbDppmsOK4/VyiDK864MBI/AAAAAAACHPs/X5ALH_ij9hQ8LsqFJ5UBFzkp-oyj9fmHgCLcB/s72-c/IMG-20160503-WA0143.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/wanahabari-iringa-waadhimisha-siku-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/wanahabari-iringa-waadhimisha-siku-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago