Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Tozo daraja la Nyerere kuanza Jumamosi

Katibu mkuu: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhu...

Katibu mkuu: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutozwa kwa vyombo vya usafiri vitavyopita katika Daraja la Nyerere kuanzia jumamosi ya Mei 14.
(Picha na Raymond Mushumbusi) MAELEZO
---
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.
 
Akizungumzia na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa kuanzia  siku   hiyo , vyombo  vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.
 
“ Tumeanza kutoza tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri  tangu Aprili 19 mwaka huu na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi Nyamhanga.
 
Mhandisi  Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600, waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa kulipia Sh.1500.
 
Mabasi yanayobeba  abiria 15 yatalipia  Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15  Sh. 5,000  na yale yanayobeba  abiria zaidi  ya 29 yatalipia Sh. 7,000.
 
Aidha magari yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000  na yale yenye  tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.
 
Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Tozo daraja la Nyerere kuanza Jumamosi
Tozo daraja la Nyerere kuanza Jumamosi
https://3.bp.blogspot.com/-jsAepGAeZLU/VzHuVVSQl9I/AAAAAAADhb0/zZoW4jY2zcsbjPyvFyaXfCizqub2qECxgCKgB/s640/T.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-jsAepGAeZLU/VzHuVVSQl9I/AAAAAAADhb0/zZoW4jY2zcsbjPyvFyaXfCizqub2qECxgCKgB/s72-c/T.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/tozo-daraja-la-nyerere-kuanza-jumamosi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/tozo-daraja-la-nyerere-kuanza-jumamosi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago