Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TAARIAFA YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA INAYOADHIMISHWA TAREHE 15 MEI, 2016

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA   WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO Tarehe 15 Mei ya kila mwaka, Tanzania...

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
 WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Tarehe 15 Mei ya kila mwaka, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia. Maadhimisho haya yametokana na Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa Na. 47/257 la tarehe 20 Septemba, 1993, linalohimiza nchi wanachama kuwa na siku maalum ya Familia.

Lengo la Maadhimisho haya ni kutambua umuhimu wa familia kama kitovu cha Maendeleo katika jamii na pia kuzienzi familia kwa kuzipa siku maalum ya maadhimisho kuwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo. Aidha, kutambua kuwa uzingatiaji wa masuala ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupaswa kujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya familia kwa ajili ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika maendeleo ya taifa lao.  Mwaka 2016, Tanzania itaadhimisha siku hii katika ngazi ya mikoa na wilaya kulingana na taratibu na mazingira ya mikoa husika. Maendeleo ya nchi hayawezi kufikiwa kama familia hazitakuwa na afya bora. Kwa kutambua hili, Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia 2016 inasema: 

“Familia Yenye Afya Bora ni Mwanga wa Maendeleo”. Kauli mbiu hii inalenga kuchochea mafanikio ya malengo ya Maendeleo Endelevu yatakayozingatia uboreshaji wa huduma ya afya bora ya familia zetu, kuwa na malezi bora ya watoto na kusisitiza utunzaji wa afya ya wanajamii wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu. Wizara inatoa wito kwa kila mwanafamilia kushiriki maadhimisho ya Siku hii muhimu kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Aidha, tunaomba vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa Maadhimisho haya ili kuharakisha uboreshaji wa afya za wanafamilia wote katika nchi yetu.  

 Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TAARIAFA YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA INAYOADHIMISHWA TAREHE 15 MEI, 2016
TAARIAFA YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA INAYOADHIMISHWA TAREHE 15 MEI, 2016
https://3.bp.blogspot.com/-e9spVIod0sE/VzHvzcW-3kI/AAAAAAADhcA/Wvzi1Js6dpANIbW8PL77FGiWp2V8vrd7gCLcB/s320/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
https://3.bp.blogspot.com/-e9spVIod0sE/VzHvzcW-3kI/AAAAAAADhcA/Wvzi1Js6dpANIbW8PL77FGiWp2V8vrd7gCLcB/s72-c/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/taariafa-ya-wizara-ya-afya-maendeleo-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/taariafa-ya-wizara-ya-afya-maendeleo-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago