Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo. -- Na Woinde Shizza,Arusha Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi...

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.
--
Na Woinde Shizza,Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubui .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku akuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.


“mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo piamtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwaviongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama faccebook.

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria .

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatuakali za kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40),  mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI.
MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI.
https://2.bp.blogspot.com/-Ch1rdl7d8og/Vz7_NQx3S7I/AAAAAAADhn0/oOE2e_MR7jkRuZ63lQ33-n1LA_o652VaQCLcB/s640/proxy.jpeg
https://2.bp.blogspot.com/-Ch1rdl7d8og/Vz7_NQx3S7I/AAAAAAADhn0/oOE2e_MR7jkRuZ63lQ33-n1LA_o652VaQCLcB/s72-c/proxy.jpeg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/mwanafunzi-mbaroni-kwa-kumtukana-rais.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/mwanafunzi-mbaroni-kwa-kumtukana-rais.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago