Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Mtanzania achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (AALCO)

Profesa Kennedy Gastorn, Katibu Mkuu mpya AALCO  Mkurugenzi wa masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa K...

Profesa Kennedy Gastorn, Katibu Mkuu mpya AALCO 

Mkurugenzi wa masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kennedy Gastorn amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria katika nchi za Asia na Afrika-‘Asian-African Legal Consultative Organisation-AALCO’.

Profesa Gastorn alichaguliwa kwa kauli moja wakati wa Mkutano wa 55 wa Jumuiya hiyo yenye jumla ya nchi wanachama 47 uliofanyika Mjini New Delhi, India tarehe 17 Mei, 2016 na kuhudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Baraka Luvanda. 

Aidha, Profesa Gastorn ambaye alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Tanzania na kupitishwa na Umoja wa Afrika, anachukua nafasi ya Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Profesa Rahmat Mohamad wa Malaysia ambaye muda wake unamalizika rasmi ifikapo mwezi Agosti, 2016 na Profesa Gastorn anatarajia kukabidhiwa madaraka hayo mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2016.

Mkutano wa Jumuiya ya AALCO ulifanyika kuanzia tarehe 16 Mei na kumalizika tarehe 20 Mei, 2016.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 20 Mei, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Mtanzania achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (AALCO)
Mtanzania achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya masuala ya Kisheria katika Nchi za Asia na Afrika (AALCO)
https://3.bp.blogspot.com/-oXfD_z0nVT8/Vz8Bih37nyI/AAAAAAADhoM/QUAGc1XPB3EXFAwVoNaDxy677Y8kulnAQCLcB/s640/gastorn.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-oXfD_z0nVT8/Vz8Bih37nyI/AAAAAAADhoM/QUAGc1XPB3EXFAwVoNaDxy677Y8kulnAQCLcB/s72-c/gastorn.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/mtanzania-achaguliwa-kuwa-katibu-mkuu.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/mtanzania-achaguliwa-kuwa-katibu-mkuu.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago