Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MHIFADHI MWANDAMIZI TANAPA ASHIKILIWA BAADA YA KUKUTWA NA JINO LA TEMBO.

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUSHIKILIWA NA KIKOSI KAZI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI KWA MHIFADHI...


HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUSHIKILIWA NA KIKOSI KAZI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI KWA MHIFADHI MWANDAMIZI GENES SHAYO

Mhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Genes Shayo (60) anashikiliwa na Kikosi Kazi Maalum cha kupambana na ujangili nchini kufuatia taarifa za kuhusishwa kwake na upatikanaji wa jino la tembo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Shirika la Hifadhi za Taifa kupitia taratibu za utendaji kazi lilipokea taarifa za kintelijensia tarehe 14.05.2016 zikimhusisha mwananchi mmoja mkazi wa Ngarenanyuki, Arumeru Emmanuel Nassari (46) ambaye ni Mchungaji wa Kanisa TAG kumiliki jino la tembo na kuwa alihitaji kupata mtu wa kufanya naye biashara. Baaada ya kupata taarifa hizi shirika liliwasiliana na Kikosi Kazi Maalum cha Kitaifa kinachohusika na masuala ya ujangili ili kushirikiana kwa ajili ya ufuatiliaji.

Kikosi Kazi hiki mara baada ya kupata taarifa hizi kiliendelea na taratibu zake za kiuchunguzi na baada ya ufuatiliaji walifanikiwa kumkamata Emmanuel Nassari tarehe 15.05.2016 akiwa na jino moja la tembo ambapo katika mahojiano yaliyofanyika alimhusisha Mhifadhi Mwandamizi wa TANAPA Genes Shayo kuwa anazo taarifa za yeye kuwa na jino hilo na hivyo kukamatwa tarehe 16.05.2016 kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea kutoa wito kwa raia wema wa nchi hii kuendelea kutoa taarifa za kufichua vitendo vya ujangili na kwamba halitasita kuchukua hatua stahiki kwa yeyote anayehusika na vitendo hivi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wake watakaobainika kisheria kuhusika na vitendo hivi.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
S.L.P 3134
ARUSHA
Simu: +255 027 254 4082
Baruapepe: dg@tanzaniapaks.go.tz
Wavuti: www.tanzaniaparks.go.tz

23.05.2016


COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MHIFADHI MWANDAMIZI TANAPA ASHIKILIWA BAADA YA KUKUTWA NA JINO LA TEMBO.
MHIFADHI MWANDAMIZI TANAPA ASHIKILIWA BAADA YA KUKUTWA NA JINO LA TEMBO.
https://2.bp.blogspot.com/-epF7any9lSk/V0RgkYOvsZI/AAAAAAAAdHg/MT1VIcm0QLsy3AX6NWA1QoL_RziJLf8nACLcB/s1600/download%2B%25281%2529.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-epF7any9lSk/V0RgkYOvsZI/AAAAAAAAdHg/MT1VIcm0QLsy3AX6NWA1QoL_RziJLf8nACLcB/s72-c/download%2B%25281%2529.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/mhifadhi-mwandamizi-tanapa-ashikiliwa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/mhifadhi-mwandamizi-tanapa-ashikiliwa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago