Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA

kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo   Na Woinde Shizza,Arusha Kufuatia  zoezi la kuhakiki  silaha linaloendelea ...
kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo

 
Na Woinde Shizza,Arusha
Kufuatia  zoezi la kuhakiki  silaha linaloendelea  hapa nchini jeshi la polisi mkoani Arusha  limefanikiwa  kuhakiki jumla ya silaha 2640  na  jumla ya silaha 36 zilizosalimishwa zimefutiwa leseni za umiliki kutokana na sababu mbalimbali .Akiongelea swala hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa silaha  silaha hizo zimebaki chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo na baadhi ya wamiliki kupitisha umri wa kumiliki silaha  ,wengine wakiwa wagonjwa  pamoja na wengine kukosa sifa ya kumiliki silaha  hizo.Alisema kuwa umri wa kumiliki silaha mwisho ni miaka 70  ambapo kuna baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanamiliki silaha hizo tayari wameshafikia ukomo wa umri wa kumiliki silaha hizo kisheria.Aidha alisema pia kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanamiliki silaha zaidi ya moja bila sababu yeyote nao wamenyang’anywa huku wengine wakiwa wamechukuwa silaha hizo bila kujua matumizi halali ya umiliki wa silaha hizo.Alitaja aina ya silaha ya silaha mbalimbali ambazo  tayari zimekaguliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kuwa ni  bastola 1434,Raifo 540 pamoja na Shortigun 666.

Alisema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kuhakiki silaha hizo hivyo wananchi wote ambao wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria .Mkumbo pia aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata mafunzo kwanza kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi arudi  kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi juu ya matumizi sahihi ya silaha.


COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA
JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2016/04/15/MKUMB.jpg?itok=K11L7msU
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/jumla-ya-silaha-36-zazuiliwa-na-jeshi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/jumla-ya-silaha-36-zazuiliwa-na-jeshi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago