Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI MSIMBAZI BONDENI.

Maelezo ya picha kushoto :  Fundi kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa...


Maelezo ya picha kushoto:  Fundi kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa umeunganishwa kwenye kisima kinyume na utaratibu ambapo walikuwa wakitumia huduma ya Maji bila kuwa na mita wala akaunti namba ambapo walinzi jengo hilo awali walidai maji wanayotumia ni ya kisima kwenye jengo lilipo eneo la Msimbazi Bondeni jijini Dar es Salaam.Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji katika eneo la kata ya Ilala mchikichini mtaa wa Msimbazi Bondeni ambapo walinzi wa jengo hilo walikuwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu nakujifanya kuwa wanatumia Maji ya Kisima.

Akizungumza kwenye eneo la tukio Afisa biashara msidaizi  wa Dawasco Ilala Sezi Mavika amesema kuwa jengo hilo haliishi mtu bali wapo walinzi tu na mwenye jengo hilo anajulikana kwa jina moja tu la Duncan na kueleza kuwa walinzi hao wamejiunganishia huduma ya Maji kwa muda mrefu na wanatumia kumwagilia maua pamoja nakufanyia shughuli za usafi kwenye jengo hilo.

“Tumekuta walinzi wameunganisha huduma ya Majisafi kwenye jengo hili linalomilikiwa na bwana Duncan ambapo wamejiunganishia kwa kupitisha kwenye kisima kisichofanya kazi nakudai kuwa Maji wanayotumia niya Kisima ndipo tulipo shirikisha ofisi ya serikali ya mtaa nakuweza kukagua nakuona kuwa wajiunganishia maji yetu na hawana mita wala akaunti namba na watumia kwa muda mrefu huduma ya maji ya Dawasco” alisema Sezi.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa serikali ya mtaa ya Msimbazi Bondeni bi Cecilia Kasele ametoa rai kwa wananchi wote wa mtaa wao kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na kuwasihi wananchi kuwataja wezi wa Maji kwenye maeneo yao kwani hao ndio wanaofanya wakose huduma bora ya Maji.

“Napenda kuwasihi wananchi wote wa mtaa wangu kujiepusha na tabia ya wizi wa Maji na pia nawasihi wale wote wanaofahamu wezi wa Maji kujitokeza na kuwataja kwani hao wezi ndio wanasabisha Dawasco kutokuweza kutoa huduma bora kutokana nakuhujumiwa na watu wachache” alisema Kasele.

Dawasco inaendelea na operesheni yake ya kukamata wezi wa Maji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na hivyo inawasihi wananchi wote waliojiunganisha huduma ya Maji kinyume na utaratibu wajitokeze nakusajiwa kihalali pia watumie fursa hii ya zoezi la kuunganishia wateja wapya kupata huduma ya Maji kihalali, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaokamatwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu.

Mwisho.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI MSIMBAZI BONDENI.
DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI MSIMBAZI BONDENI.
https://1.bp.blogspot.com/-GfgCvGCCLMk/V0v_WcljO9I/AAAAAAAAdP8/7fDgs9g_3d0JgorvsyDNHqA2GikfSkI0gCLcB/s640/IMG_6127.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-GfgCvGCCLMk/V0v_WcljO9I/AAAAAAAAdP8/7fDgs9g_3d0JgorvsyDNHqA2GikfSkI0gCLcB/s72-c/IMG_6127.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/05/dawasco-yabaini-wizi-wa-maji-msimbazi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/05/dawasco-yabaini-wizi-wa-maji-msimbazi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago