Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO AFRIKA MASHARIKI

Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari...

DSC_0002
Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Rabi Hume wa Modewjiblog)

Wananchi wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia nafasi za kufanya baishara zilizopo kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana na kuwepo makubaliano ambayo yanawapa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara kwa uhuru.

Hayo yamesema na Mbuge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na kusema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na shirikisho wa kisiasa.

Amesema kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya baishara katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza bishaa zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Huu ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya baishara kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo zilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo lakini tumejipanga katika hilo,” amesema Nyerere.
Amesema kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano huo.

Amesema programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.

Pia Nyerere amewataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.
Shyrose Bhanji
Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza jambo.
DSC_0018
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakichukua habari.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO AFRIKA MASHARIKI
WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO AFRIKA MASHARIKI
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/04/DSC_0002.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/watanzania-watakiwa-kuchangamkia-fursa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/watanzania-watakiwa-kuchangamkia-fursa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago