Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa Kwa Umma Kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya;

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Ma...

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon. 

Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha  Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Mashtaka hayo yalisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro. Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali Herman Tibabyekomia, Christopher Msigwa na  Mwendesha Mastaka wa TAKUKURU Stanley Luoga. Washtakiwa wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Ringo Tenga, Rosai Mbwambo, Semo na Nyaisa. 

Washitakiwa wote watatu wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani  Kifungu Na. 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Kinazuia utoaji wa dhamana kwa washtakiwa wa Utakatishaji wa fedha haramu. Kesi hii itatajwa tena tarehe 8/4/2016.

IMETOLEWA NA 
OFISI YA AFISA UHUSIANO 
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU 
1 APRIL, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa Kwa Umma Kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya;
Taarifa Kwa Umma Kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya;
https://3.bp.blogspot.com/-SNo21XK95i8/Vv6RfRt_BfI/AAAAAAADgkQ/oDz_pGzcLM0wBF44Mw-TmTZ8cLsF6OZOw/s640/Screen%2BShot%2B2016-03-30%2Bat%2B6.35.08%2BPM.png
https://3.bp.blogspot.com/-SNo21XK95i8/Vv6RfRt_BfI/AAAAAAADgkQ/oDz_pGzcLM0wBF44Mw-TmTZ8cLsF6OZOw/s72-c/Screen%2BShot%2B2016-03-30%2Bat%2B6.35.08%2BPM.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/taarifa-kwa-umma-kutoka-taasisi-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/taarifa-kwa-umma-kutoka-taasisi-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago