Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

PICHA NA TAARIFA NA IKULU:RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania ...

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa  Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani.
 Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam.Picha na IKULU
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe ameapishwa leo tarehe 19 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Batilda Salha Burian ambaye Mkataba wake  umemalizika.Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Mheshimiwa Chikawe ameahidi utumishi uliotukuka na kuiunganisha vyema Tanzania na Japan hususani katika masuala ya kiuchumi.

Mheshimiwa Chikawe ametoa wito kwa watanzania wote hasa waishio Japan na nchi nyingine zinazotumia Ofisi ya Ubalozi huo wa Tanzania, kuutumia vizuri ubalozi huo ili kunufaika na fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.

Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, pia unatoa huduma za kibalozi katika nchi za Korea Kusini, New Zealand, Papua New Guinea na Australia.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
19 Aprili, 2016.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: PICHA NA TAARIFA NA IKULU:RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN
PICHA NA TAARIFA NA IKULU:RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN
https://1.bp.blogspot.com/-6-9u6mR4myw/VxZK33Cg9UI/AAAAAAADhJM/W3_axhUZltQORIo2cLBO-LHrQoZUTMbhgCLcB/s640/1%252B%2525282%252529.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-6-9u6mR4myw/VxZK33Cg9UI/AAAAAAADhJM/W3_axhUZltQORIo2cLBO-LHrQoZUTMbhgCLcB/s72-c/1%252B%2525282%252529.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/picha-na-taarifa-na-ikulurais-dkt.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/picha-na-taarifa-na-ikulurais-dkt.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago