Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Naibu Waziri Annastazia atoa maagizo Kiwanja cha TBC kilichopo Kimani Wilaya ya Kisarawe kupatiwa Hati

  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi Nahya Ma...

 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi Nahya Mansour alipowasili katika Ofisi za Wilaya hiyo kwa ziara ya kikazi ya kukagua Viwanja vya makazi vya Shirika la Utangazi  Tanzania (TBC) vilivyopo wilayani humo.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Kisarawe(Hawapo pichani) alipofika katika ofisi za Wilaya hiyo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akipokea taarifa ya kiwanja cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kilichopo eneo la Kimani katika Wilaya ya Kisarawe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bi Mwanamvua Mrin
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Meneja Miradi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Mackselin Chota.
---
Na Shamimu Nyaki, WHUSM
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura amemuagiza Meneja wa Miradi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC ) Bw. Mackselin Chota kuhakikisha kiwanja  Na.1 Kitalu “B” kilichopo eneo la Kimani wilaya ya Kisarawe kinapatiwa Hati Miliki  ili kuepusha kuvamiwa pamoja na migogoro inayoweza kutokea.
 
Agizo hilo amelitoa jumamosi wakati alipotembelea kiwanja hicho na kueleza kuwa kiwanja hicho ni lazima kiendelezwe kwa ajili ya kuwasaidia wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo kiwanja hicho kilitafutwa kwa dhumuni hilo.
 
“Naishukuru Halmashauri kwa  kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo,hivyo natoa siku saba kwa  idara ya Miradi ya TBC kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha kiwanja hicho  kinapatiwa Hati”.Alisema Mhe.Annastazia.
 
Aidha amewataka kuwasilisha gharama zilizotumika katika ujenzi wa nyumba zilizopo katika eneo hilo na wapi zimetoka na sababu zilizosababisha ujenzi huo kukwama kwa zaidi ya miaka mitatu.
Akitoa maelezo kuhusu Kiwanja hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa kiwanja hicho kilipimwa  na ramani yake ya upimaji ilipata kibali cha Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kusajiliwa kwa namba 68480,ramani namba E 292/83 ya tarehe 22 februari, 2012.
 
“Taratibu za umilikishwaji zilifanyika kwa kuandaliwa gharama za kulipia kabla hati haijaandaliwa,malipo hayo yalifanywa na TBC kupitia NMB na kuwasilisha fomu ya malipo hayo(Bank pay in slip)”.Alisema Bi Mwanamvua.
 
Naye Meneja wa Miradi wa Shirika la Utangazaji Tanzania  Bw.Mackselin Chota amesema kuwa Shirika hilo lina jumla ya viwanja 55 nchi nzima,ambavyo 19 kati ya hivyo vina Hati miliki ambapo katika mkoa wa Pwani kuna kiwanja kimoja, Dar es Salaam viwanja vitano ambavyo viko Pugu Road,Kunduchi, na TAZARA, Mikocheni na Sinza.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Naibu Waziri Annastazia atoa maagizo Kiwanja cha TBC kilichopo Kimani Wilaya ya Kisarawe kupatiwa Hati
Naibu Waziri Annastazia atoa maagizo Kiwanja cha TBC kilichopo Kimani Wilaya ya Kisarawe kupatiwa Hati
https://3.bp.blogspot.com/-naL3fNrGO0o/Vwy8BYAhaaI/AAAAAAADg9Y/yFLcmcXWihMcMAIwgzBIJqKNPFgnPxMPwCLcB/s640/KISA1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-naL3fNrGO0o/Vwy8BYAhaaI/AAAAAAADg9Y/yFLcmcXWihMcMAIwgzBIJqKNPFgnPxMPwCLcB/s72-c/KISA1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/naibu-waziri-annastazia-atoa-maagizo.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/naibu-waziri-annastazia-atoa-maagizo.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago