Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MKURUGENZI WA HALMASHAURI ATAKAESHINDWA KUTENGA ASILIMIA KUMI KWA AJILI YA WANAWAKE NA VIJANA ATAONDOLEWA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU  WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa...

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
 WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mkurugezi yeyote wa Halmashauri nchini atakayeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana ataondolewa.

Amesema suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima na si hiari.Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo leo (10 Aprili, 2016) alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema ambako lifanya mikutano ya hadhara.

“Halmashauri ambayo itashindwa kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safariiri,” amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Waziri Mkuu, Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.

Pia Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.Amesema fedha hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa amesema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.

Imetolewa na 
Ofisi ya Waziri Mkuu

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MKURUGENZI WA HALMASHAURI ATAKAESHINDWA KUTENGA ASILIMIA KUMI KWA AJILI YA WANAWAKE NA VIJANA ATAONDOLEWA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI ATAKAESHINDWA KUTENGA ASILIMIA KUMI KWA AJILI YA WANAWAKE NA VIJANA ATAONDOLEWA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
https://3.bp.blogspot.com/-DO5x5nTXJsg/Vwtfh2tEZ4I/AAAAAAADg5g/25AfPVK0xssVdT6Xnan4G6qS6AbD5UqNQ/s1600/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
https://3.bp.blogspot.com/-DO5x5nTXJsg/Vwtfh2tEZ4I/AAAAAAADg5g/25AfPVK0xssVdT6Xnan4G6qS6AbD5UqNQ/s72-c/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/mkurugenzi-wa-halmashauri-atakaeshindwa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/mkurugenzi-wa-halmashauri-atakaeshindwa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago