Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Kamati ya Afya ya Bunge Yaitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Daktari wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara akiwaongoza wabunge kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na madaktari n...

Daktari wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara akiwaongoza wabunge kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na madaktari na wauguzi wa idara hiyo jana
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangallah akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ambayo imeitembelea jana hospitali hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa, Lawrence Museru akifafanua jambo kwa Kamati ya Bunge ya Afya kuhusu huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wa akili.
 Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Afya Akili, Dk Frank Massawe akiwaeleza wabunge wa Kamati ya Afya jinsi idara hiyo inavyotoa tiba kwa wagonjwa wa akili.
 Dk Upendo Ndara wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali akiewaeleza wabunge wa Kamati ya Afya juu ya upanuzi wa jengo la kuwahudumia wagonjwa wa dharura na ajali kwenye hospitali hiyo.
 Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare (mwenye koti) akiwaeleza wabunge wa Kamati ya Afya jinsi mashine ya CT- SCAN inavyochukua vipimo mbalimbali kwa wagonjwa. Dk Lwakatare amewaeleza wabunge hao kwamba mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kugundua matatizo ya wagonjwa.
Dk. Upendo Ndara wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali akiwaeleza wabunge wa Kamati ya Afya jinsi idara hiyo inavyowahudumia wagonjwa wa dharura na ajali wanaofikishwa hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 
---
 
Na John Stephen

Kamati ya Afya ya Bunge leo imeitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kukagua huduma  mbalimbali za afya zinazotolewa na hospitali hiyo.

Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Joseph Serukamba  akiwamo Mussa Azzan Zungu na wabunge wengine wa kamati hiyo.

Wabunge hao wametembelea Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Idara ya Magonjwa ya Akili, Idara ya Mionzi na Wodi ya Mwaisela na chumba cha kuchakacha gesi ambayo inatumika wakati wa kutoa tiba kwa wagonjwa mbalimbali.


Daktari wa magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara amewaeleza wabunge hao jinsi madaktari na wauguzi wanavyowahudumia wagonjwa wanaofikishwa kwenye idara hiyo, changamoto na jinsi wanavyofanikiwa kuokoa maisha ya wagonjwa wa ajali na wagonjwa wengine.

Pia, Dk Upendo ameelezea juhudi kubwa zinazofanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) katika kupanua jengo la idara hiyo ili kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa.

Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Frank Massawe amewaeleza wabunge mafanikio yaliopatikana baada ya wagonjwa wa akili kupatiwa matibabu na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Kamati ya Afya ya Bunge Yaitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Kamati ya Afya ya Bunge Yaitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
https://4.bp.blogspot.com/-nx4wzMW9xC4/VwNofPqls2I/AAAAAAADgrw/QlyjUupTEOco7mg-pq6qnWfsJYaD2_I-Q/s640/002.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-nx4wzMW9xC4/VwNofPqls2I/AAAAAAADgrw/QlyjUupTEOco7mg-pq6qnWfsJYaD2_I-Q/s72-c/002.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/kamati-ya-afya-ya-bunge-yaitembelea.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/kamati-ya-afya-ya-bunge-yaitembelea.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago