Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

JOKATE NA MO DEWJI FOUNDATION KUJENGA KIWANJA CHA MICHEZO SEKONDARI YA JANGWANI

Mwanzilishi wa ujenzi huo, Jokate Mwegelo akiandika jambo wakati ujenzi wa kiwanja ukiendelea. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya W...

Jokate
Mwanzilishi wa ujenzi huo, Jokate Mwegelo akiandika jambo wakati ujenzi wa kiwanja ukiendelea.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Taasisi ya Mo Dewji.

Akizungumza na Mo Blog, Jokate amesema ujenzi wa kiwanja hicho cha michezo ni sehemu ya mipango aliyokuwa nayo baada ya kuanzisha mwaka jana bonanza la Kidoti ambalo lilikuwa na malengo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri kimasomo na kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao.

Jokate amesema ameamua kuanza na shule ya Jangwani kwa kutambua kuwa shule hiyo ina hosteli za wanafunzi walemavu na wamekuwa wakipata shida kupata viwanja vya michezo hivyo kupitia kiwanja hicho wataweza kushiriki michezo kwa urahisi zaidi.

“Pale Shule ya Jangwani kuna wanafunzi walio na ulemavu na kama unavyojua mlemavu anatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka afya yake vizuri na kama wakitaka kushiriki michezo hadi waende Gymkhana lakini tunawajengea uwanja wa Basketball na Netball,” amesema Jokate wakati akifanya mahojiano na Mo Blog.

Ameongeza kuwa ili kufanikisha ujenzi huo alizungumza na Mohammed Dewji ambaye alikubali kutoa Milioni 10 kupitia Taasisi yake ya Mo Dewji na hivyo kuanza kufanyika kwa ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi wa Jangwani kushiriki michezo tofauti na hapo awali.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa viwanja vya michezo utakuwa endelevu katika shule za serikali ambazo bado hazijawa na viwanja na baada ya kukamilika kwa ujenzi katika shule ya Jangwani amepanga kufanya ujenzi wa viwanja vya michezo katika Shule ya Sekondari Kinyerezi na Shule ya Sekondari Maposeni iliyopo wilayani Peramiho, Ruvuma.
14581134867112
Ujenzi wa kiwanja cha michezo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani ukiendelea
IMG_3708
IMG_3868
IMG_3869
IMG_3872
IMG_3875
IMG_3878
IMG_3883
IMG_3884
IMG_3880
Jokate Mwegelo akibadilishana mawazo na fundi anayejenga uwanja huo wa michezo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: JOKATE NA MO DEWJI FOUNDATION KUJENGA KIWANJA CHA MICHEZO SEKONDARI YA JANGWANI
JOKATE NA MO DEWJI FOUNDATION KUJENGA KIWANJA CHA MICHEZO SEKONDARI YA JANGWANI
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/04/IMG_3886-1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/jokate-na-mo-dewji-foundation-kujenga.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/jokate-na-mo-dewji-foundation-kujenga.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago