Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

GSM WASAIDI KITENGO CHA MOI KUWEKA KAMBI YA OPARESHENI YA WATOTO WENYE MGONGO WAZI NA WENYE VICHWA VIKUBWA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusaidia ka...


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusaidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba. 
--
 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya  watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu  wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.

Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha  njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.

‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane  ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.

Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.

Afisa  Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni  hiyo.

Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga  Mei 2 hadi 4,  Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma  10  hadi 13, Morogoro Mei 15  hadi 17 .

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: GSM WASAIDI KITENGO CHA MOI KUWEKA KAMBI YA OPARESHENI YA WATOTO WENYE MGONGO WAZI NA WENYE VICHWA VIKUBWA.
GSM WASAIDI KITENGO CHA MOI KUWEKA KAMBI YA OPARESHENI YA WATOTO WENYE MGONGO WAZI NA WENYE VICHWA VIKUBWA.
https://4.bp.blogspot.com/-D987EmQedWQ/VxePzRHOWmI/AAAAAAADhKE/EBha4H4Gj3gqZzDsR6akReIBTi-odEk2wCLcB/s640/DSCF6374.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-D987EmQedWQ/VxePzRHOWmI/AAAAAAADhKE/EBha4H4Gj3gqZzDsR6akReIBTi-odEk2wCLcB/s72-c/DSCF6374.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/04/gsm-wasaidi-kitengo-cha-moi-kuweka.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/04/gsm-wasaidi-kitengo-cha-moi-kuweka.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago