Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba  (kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kita...

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba  (kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa wakati akiizindua rasmi Dar es Salaam leo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI). Kushoto ni Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour.

 Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa mada kuhusu zao la muhogo na changamoto za magonjwa yanayolishambulia.
 Baadhi ya wanakamati hao wakiwa ukumbini katika hafla 
hiyo ya uzinduzi.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa bize wakati wa uzinduzi huo.
 Wajumbe wa kamti hiyo
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo wa uzinduzi 
Mkutano ukiendelea.
Waziri Makmba (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI. Kutoka kushoto ni  Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru, Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour na Profesa Raphael Chibunda.
Picha ya pamoja na Waziri Makamba.
Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Makama na wajumbe wa kamati mpya jinsi maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI inavyofanya kazi.
Mimea mbalimbali inayofanyiwa utafiti ikiwa katika chupa maalumu katika maabara hiyo.
Mbegu ya migomba iliyooteshwa baada ya kufanyiwa utafiti katika kituo hicho cha MARI.
---
Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao na kuisaidia serikali.

Makamba alitoa mwito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

"Tengenezeni mpango kazi wenu ili serikali iufahamu na kuweza kuwasaidia kifedha endapo utakwama badala ya kukaa bila ya kuwa na dira na kusubiri kufanya mikutano yenu ya kupitisha jambo fulani mara tatu katika kipindi cha miaka nane" alisema Makamba.

Alisema kamati hiyo ni ya muhimu sana katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe wa kamati hiyo na wananchi kwa ujumla.

Alisema Tanzania ni nchi mwanachama wa mkataba wa bioanuai wenye malengo makuu matatu,  Hifadhi ya bioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai na mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yake.

Alisema Tanzania iliridhia mkataba huo mwezi Machi, 1996 ili kushirikiana na Jumuia ya Kimataifa katika kutekeleza malengo yaliyotajwa.

Alisema alisema changamoto kubwa ya teknolojia hiyo ya bioteknolojia ya kisasa bado kuna wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea ambazo ni mzio, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani, usugu wa dawa kwa matibabu ya magonjwa, wakulima kutegemea mbegu za kununua kila na madhara mengine ambayo kwa sasa hayajawa bayana.

Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru alisema wamejipanga kujenga kituo kikubwa cha utafiti kitakacho gharimu dola za Marekani 556,000.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda alisema ili wakulima waweze kufanikiwa katika kilimo chao ni vizuri wakawa wanazingatia ushauri wa wataalamu ambao wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali ambazo huwapelekea wao kwa matumizi ya kilimo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
WAZIRI JANUARY MAKAMBA AZINDUA KAMATI YA KITAIFA YA MATUMIZI SALAMA YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://1.bp.blogspot.com/-2Ol2MJwpRPs/VtbTiXcRD3I/AAAAAAAAVcI/FhRJuIMur4c/s640/1.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-2Ol2MJwpRPs/VtbTiXcRD3I/AAAAAAAAVcI/FhRJuIMur4c/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/waziri-january-makamba-azindua-kamati.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/waziri-january-makamba-azindua-kamati.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago