Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAKALA WA MAJENGO TANZANIA YAIPA MKATABA YONO AUCTION MART WA KUKUSANYA MADENI NCHINI

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ,  Arch. Elius Mwakalinga (kushoto), akikabidhiana hati ya mkataba na Mwakilishi wa ...

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ,  Arch. Elius Mwakalinga (kushoto), akikabidhiana hati ya mkataba na Mwakilishi wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kampuni hiyo kushinda zabuni ya kukusanya madeni ya TBA kuanzia leo.
 Taswira meza kuu katika mkutano huo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) , Arch Elius Mwakalinga (katikati), akizungumza katika mkutano huo kabla ya kutiliana saini na kampuni ya Yono. Kushoto Ofisa wa Idara ya Manunuzi, Mariam Kazoba.
 Ofisa wa Idara ya Manunuzi wa TBA, Mariam Kazoba, akitoa ufafanuzi mbalimbali katika mkutano huo.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela (kulia), akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema Yono wamejipanga kuwafikia wadaiwa wote wa TBA.
 Mkataba akisainiwa kwa pande zote.
 Wanahabari wakiwa bize kuchukua taarifa hiyo.
Ofisa Habari wa TBA, Mirembe Dashina (kulia), akiteta jambo na mwenzake katika mkutano huo.
-

Na Dotto Mwaibale

WAKALA  wa Majengo Tanzania (TBA), umecharuka kwa kuingia mkataba na Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd ili kusaidia kukusanya madeni ya wadaiwa sugu ambao walikopa nyumba.

Wakati huo huo mwakilishi wa kampuni hiyo ya udalali ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela ametoa siku tatu kwa wadaiwa wote wa TBA kuhakikisha wanalipa fedha hizo kabla ya kufikiwa na kampuni hiyo ambayo Jumatano ya Machi 16 mwaka huu itaanza rasmi kazi ya kuwaondoa katika nyumba za wakala huo watumishi wote wanaodaiwa kwa kufuata sheria kama inavyoelekeza.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa kutiliana saini na kampuni hiyo ya udalali kwa ajili ya kukusanya fedha kutoka kwa wadeni wa wakala huo  Mtendaji Mkuu wa TBA ,  Elius Mwakalinga alisema wamefia hatua hiyo baada ya kuona wadaiwa wao ambao wengi wao ni kutoka sekta za serikali kushindwa kulipa fedha hizo.

"Tumeingia mkataba na Kampuni ya Yono Auction Mart baada ya kushinda zabuni ambayo tulitangaza Februari 23,2016 na sasa kazi yote ya ukusanyaji wa fedha hizo itafanywa na kampuni hiyo" alisema Mwakalinga.

Mwakalinga alisema fedha nyingi za wakala huo zipo mikononi mwa wadaiwa wao ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma ni shilingi.Bilioni 6 na kwa waliokopa ni sh.milioni 800 huku fedha zinazodaiwa kwa ajili ya kutoa ushauri mbalimbali wa ujenzi ni sh.bilioni 6.95.

Mwakilishi wa kampuni  ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scollastica Kevela alisema wametoa siku tatu kwa wadaiwa wote kuhakikisha wanalipa fedha hizo vinginevyo watafikiwa na kampuni hiyo ambayo imepanga rasmi kupita kila nyumba inayodaiwa na kuwa kila muhusika atatakiwa kuilipa kampuni hiyo asilimia tano ya fedha anazodaiwa na TBA.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAKALA WA MAJENGO TANZANIA YAIPA MKATABA YONO AUCTION MART WA KUKUSANYA MADENI NCHINI
WAKALA WA MAJENGO TANZANIA YAIPA MKATABA YONO AUCTION MART WA KUKUSANYA MADENI NCHINI
https://1.bp.blogspot.com/-fPIvS1QhafI/VuK8aI0ofeI/AAAAAAAAVio/4A9eiLnzYkIGr6qADPaoybalryNzVvsug/s640/1.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-fPIvS1QhafI/VuK8aI0ofeI/AAAAAAAAVio/4A9eiLnzYkIGr6qADPaoybalryNzVvsug/s72-c/1.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/wakala-wa-majengo-tanzania-yaipa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/wakala-wa-majengo-tanzania-yaipa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago