Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe...

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA). Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi George Sambali (kushoto) wakiwa kwenye warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) warsha hiyo ilifanyika katika ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau mbali mbali wa sekta ya usafiri wa anga wakishiriki warsha ya kujadili rasimu ya Mpango wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
---- 
Wadau wa sekta ya Usafiri wa anga nchini ,wamekutana katika warsha ya siku moja kujadili rasimu ya mpango kamambe wa usafiri wa anga  yaani ( the Civil Aviation Master Plan) makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini(TCAA), Banana-Ukonga. 

Warsha  hiyo iliyowakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi  na Mawasiliano, mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga  nchini , Mamlaka ya Viwaja vya Ndege na mwenyeji Mamlaka ya Usafiri wa Anga  imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho.

Lengo la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri wa anga nchini  ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya Dunia. Kampuni hiyo ilianza kuanda rasimu hiyo mwaka 2015 kazi ambayo imefanyika kwa miezi 12. 

Akizungumza  wakati wa ufunguzi huo , katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema lengo la serikali ni kuwezesha  Tanzania kutoa huduma za usafiri wa anga  kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubaliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) pamoja na kuweka mazingira mazuri yatakayoruhusu  ushindani wa kibiashara katika sekta hii.  

Ameongeza kuwa sekta ya usafiri wa anga imekuwa ikikua , mathalani  takwimu zinaonyesha safari za ndege zimeongezeka kwa asilimia 8  katika mwaka 2015 ikilinganishwa na zile zilizofanyika mwaka 2014. Kadhalika idadi ya abiria imekuwa ikikua kwa kiwago cha asilimia 1.5- 2 kwa mwaka.  

Lengo la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri wa anga nchini  ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya Dunia.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO
WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://3.bp.blogspot.com/-PoLEbSm3g-I/VvvrbYTEwtI/AAAAAAADge8/bJURWJayDSII75peWvhhjsIjo-V4t_lNA/s640/2.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-PoLEbSm3g-I/VvvrbYTEwtI/AAAAAAADge8/bJURWJayDSII75peWvhhjsIjo-V4t_lNA/s72-c/2.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/wadau-wa-sekta-ya-usafiri-wa-anga.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/wadau-wa-sekta-ya-usafiri-wa-anga.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago