Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

UJUMBE KUTOKA KWA BI. IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO, KATIKA SIKU YA USHAIRI DUNIANI, 21 MACHI 2016

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova. --- Shakespeare, mwandishi maarufu kutoka Uingereza aliyefariki yapata miaka 400 iliyo...

The-director-general-of-UNESCO-Irina-Bokova
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova.
---
Shakespeare, mwandishi maarufu kutoka Uingereza aliyefariki yapata miaka 400 iliyopita, aliandika katika tamthilia yake inayojulikana kama “A Midsummer Night's Dream” kuwa, “Jicho la mshairi, hutazama kwa umakini na undani, kutoka mbinguni hadi duniani, na duniani hadi mbinguni. Na kama vitu vya kufikirika vusivyofahika vinavyoumbika katika mawazo, ndivyo kalamu ya mshairi inavyogeuza mawazo hayo kuwa katika maumbo yasiyoweza kudhaniwa”
Kwa kuwatambua na kuwaheshimu wanaume na wanawake, ambao chombo chao pekee ni uhuru wa kujieleza, watu wanaofikiria na kuchukua hatua, UNESCO inatambua thamani ya ushairi kama ishara ya ubunifu wa mwanadamu. Kwa kutoa umbo na maneno kwa mambo ambayo katika hali ya kawaida hayakuwa nayo, kama vile uzuri usiopimika unaotuzunguka na mateso na taabu kubwa za dunia, mashairi yanachangia upanuzi wa ubinadamu wetu, kwa kusaidia kuongeza nguvu za ubinadamu wetu, mshikamano na kujitambua.

Sauti zinazobeba ushairi husaidia kukuza upana na utofauti wa lugha na uhuru wa kujieleza. Sauti hizi hushiriki katika jitihada za kimataifa kuelekea elimu ya kisanii na usambazaji wa utamaduni. Wakati mwingine, neno la kwanza la shairi latosha kabisa kurejesha kujiamini pale mtu anapokuwa anakabiliwa na upinzani na kupelekea kuiona tena njia ya matumaini pale unapopambana na unyama. Katika zama hizi za teknolojia na uharaka wa maisha ya kisasa, ushairi hufunya nafasi kwa ajili ya uhuru na kuvinjari, hali iliyo ndani ya utu wa mwanadamu. Kutoka Arirang za huko Korea hadi Pirekua za Mexico, nyimbo za Hudhud za jamii ya watu wa Ifugao, Alardah za Saudi Arabia, Koroghlu za jamii ya watu wa Turkmenistan na maeneo ya Iran na Afghanistan, na Aitysh za watu wa Kyrgyz, kila utamaduni una aina ya sanaa yake ya ushairi inaoutumia kupeleka na kusambaza maarifa, maadili ya kijamii na kiutamaduni na kumbukumbu za pamoja, ambayo huimarisha kuheshimiana, mshikamano wa kijamii na kutafuta amani.

Leo hii, nawapongeza washairi, wasanii, waghani, na wale wote ambao sauti zao, bila ya wao wenyewe kujulikana, wamejitoa, kwa na kupitia ushairi, kutoa masomo katika hali ya taswira au ya uwazi, katika bustani au katika mitaa. Ninatoa wito kwa nchi wanachama wote wa UNESCO kuunga mkono juhudi hizi za ushairi, ambao una uwezo wa kutukusanya pamoja, bila kujali asili au imani, kwa lile lililo hasa katika kiini cha ubinadamu

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: UJUMBE KUTOKA KWA BI. IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO, KATIKA SIKU YA USHAIRI DUNIANI, 21 MACHI 2016
UJUMBE KUTOKA KWA BI. IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO, KATIKA SIKU YA USHAIRI DUNIANI, 21 MACHI 2016
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/03/The-director-general-of-UNESCO-Irina-Bokova.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/ujumbe-kutoka-kwa-bi-irina-bokova.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/ujumbe-kutoka-kwa-bi-irina-bokova.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago