Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto z...

IMG_7655
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma hiyo. (Picha na Modewjiblog)

Mwaka 2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi amesema mkutano huo unalengo wa kukutanisha wadau mbalimbali wa intaneti ili kutanua miondombinu ya intaneti katika bara la Afrika.
Amesema taasisi yake inapenda kuona huduma ya intaneti ikipatikana kwa urahisi kwa watumiaji wake Afrika na hivyo kupitia mkutano huo wataweza kutazama jinsi gani wanaweza kushirikiana na kubadilishana takwimu za watumiaji wa mitandao kwa bara zima la Afrika.

“Tunatambua kuwa watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka na kupitia mkutano huu tutaweza kuangalia jinsi gani tunaboresha huduma ya intaneti iwe bora ili iweze kutumiwa na watu wengi zaidi,” amesema Mwangi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba amesema mkutano huo una umuhimu kwa Watanzania kwa kupata fursa ya kujifunza na kubadilishana mawazo na watu kutoka mataifa mengine katika huduma ya intaneti.
Amesema kwa sasa Tanzania bado ina changamoto nyingi katika huduma ya intaneti na kupata nafasi hiyo ya kuandaa mkutano kutakuwa na faida kwa mashirika yanayotoa huduma ya intaneti ili kuwawezesha kutambua ni jinsi gani wataboresha huduma kwa wateja

“Nchi yetu inawatumiaji wengi wa intaneti ila bado kuna changamoto nyingi ikiwepo usalama wa mtandao na serikali inafanya jitihada nyingi kumaliza changamoto hizo na kupitia mkutano huu tunaamini utasaidia zaidi Watanzania kupata kitu kipya katika huduma ya intaneti,” amesema Simba.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary amesema Watanzania wengi bado hawajafahamu umuhimu wa intaneti kutokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu intaneti lakini kupitia mkutano huo ulioandaliwa na Internet Society wataweza kuapata elimu mpya kuhusu intaneti.
IMG_7593
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary.
IMG_7596
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto), Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary, Meneja Mradi wa Tanzania Internet Exchange (TIX), Frank Habicht na Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi wakizungumza jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
IMG_7603
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary akifungua mkutano huo.
IMG_7613
Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi akizungumzia mkutano wa Intaneti, AfPIF utakaofanyika nchini, Agosti, 30 - Septemba, 1
IMG_7617
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.
IMG_7629
IMG_7631
IMG_7645
IMG_7622
Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo.
IMG_7667
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2016/03/IMG_7655.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/tanzania-kuwa-mwenyeji-wa-mkutano-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/tanzania-kuwa-mwenyeji-wa-mkutano-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago