Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA-TAKUKURU JUU YA WABUNGE WATATU NA WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA LEO

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa ...


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a). Wabunge hao ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero ; Mheshimiwa Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibala.

Wabunge hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba. Akisoma mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati huo ijadiliwe tahere 16/3/2016 ipitishwe bila marekebisho.

Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia kwa dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 5. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena. 

TAKUKURU inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria. Rushwa haivumiliki!


IMETOLEWA NA 
OFISI YA AFISA UHUSIANO 
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU 
31 MACHI, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA-TAKUKURU JUU YA WABUNGE WATATU NA WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA LEO
SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA-TAKUKURU JUU YA WABUNGE WATATU NA WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA LEO
https://2.bp.blogspot.com/-JZ0vgzqsm2g/Vv0jJkfx9YI/AAAAAAADgjc/x69ap09y1QYGnMHPadXI8qbecFNIH-lRg/s1600/index.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-JZ0vgzqsm2g/Vv0jJkfx9YI/AAAAAAADgjc/x69ap09y1QYGnMHPadXI8qbecFNIH-lRg/s72-c/index.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/soma-taarifa-kwa-umma-kutoka-taasisi-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/soma-taarifa-kwa-umma-kutoka-taasisi-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago