Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SERIKALI YAPONGEZA JUHUDI ZA CHUO CHA AGHA KHAN KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali waliojumui...

DSC_8632Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
DSC_8640 DSC_8641Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
DSC_8648Baadhi ya wanafunzi na watumishi wa Chuo hicho wakiwa katika tukio hilo
DSC_8653 DSC_8654Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akisisitiza jambo..
DSC_8670Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo..
DSC_8677 DSC_8693DSC_8735Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akitoa maelezo mafupi kabla ya kuzindua rasmi jengo hilo la shule ya wauguzi na wakunga katika chuo kikuu cha Agha Khan..
DSC_8712 DSC_8710Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba ya Serikali namna Wizara Afya itakavyonufaika na wataalam wa sekta ya Afya watakaopata elimu katika shule hiyo
DSC_8737Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akifungua rasmi jengo hilo
DSC_8746 DSC_8748DSC_8721Wageni mbalimbali wakifuatilia tukio hilo
DSC_8761Msimamizi wa shule hiyo ya Uuguzi na Ukunga akitoa maelezo machache kwa wageni mbalimbali..
DSC_8751Picha ya pamoja baada ya ufunguzi huo..
DSC_8766 DSC_8772Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akiangalia namna ya vifaa vya kisasa vya kufundishia jinsi viavyotumika wakati wa kutoa huduma Hospitalini
DSC_8788Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akijaaribu kupata vipimo kuashiria ufunguzi wa jengo hilo pamoja vifaa vya kisasa vilivyowezeshwa na Serikali ya Ujerumani. Kushoto kwake ni Dk. Kigwangalla akimwelezea jambo la kitaalam juu ya vipimo hivyo.
DSC_8805Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari namna Serikali itakavyonufaika kupitia shule hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
---
 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha kuwa itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kuleta maendeleo kwenye nyanja mbalimbali hapa nchini huku ikipongeza juhudi zinazofanywa na Taasisi ya mtandao ya Agha Khan kwa jitihada zake kufundisha wataalam wa sekta ya Afya.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 31.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga katika ngazi ya digrii katika chuo cha Agha Khan, Jijini Dar es Salaam.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Chuo hicho Kikuu cha Agha Khan kwa kuanzisha shule hiyo wanaongeza idadi ya vyuo vitakavyokuwa vikizalisha kwa wingi wataalam watakaokuwa wakipta digrii kwani awali kulikuwa na upungufu mkubwa.

Jengo la Chuo hicho cha Uuguzi na Ukunga, limefanyiwa ukarabati pamoja na kupatiwa vifaa mbalimbali kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo waliwezesha kwa kugharamia ujenzi wa jengo hilo pamoja na vifaa vya kisasa vya kufundishia.

Kwa upande wake, mgeni rasmi mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani, Waziri wa Uchumi na Maendeleo, Dk. Gerd Muller ambaye alibainisha kuwa, wanataka kuona watalaama wengi wa sekta ya afya wanapata elimu ilikuondokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili wanadamu na kuongeza kuwa, bila wataalam wa tiba, Jamii haitakuwa salama.

Aidha, katika tukio hilo,wageni na viongozi mbalimbali walipata kulitembelea jengo hilo pamoja na kushuhudia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea shuleni hapo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SERIKALI YAPONGEZA JUHUDI ZA CHUO CHA AGHA KHAN KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI
SERIKALI YAPONGEZA JUHUDI ZA CHUO CHA AGHA KHAN KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI
https://i.ytimg.com/vi/4wwuHsRwvD4/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/4wwuHsRwvD4/default.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/serikali-yapongeza-juhudi-za-chuo-cha.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/serikali-yapongeza-juhudi-za-chuo-cha.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago