Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

SERIKALI YAFARIJIKA KWA USHINDI WASANII WA TUZO ZA FILAMU

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim,Majaliwa akipokea tuzo ya filamu kutoka kwa msanii Single Mtambalike aliyo...

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim,Majaliwa akipokea tuzo ya filamu kutoka kwa msanii Single Mtambalike aliyoshinda katika Tuzo za Filamu Afrika kwa mwaka 2016 zilizofanyika chini Nigeria hivi karibuni kulia ni msanii Elizabeth Michael.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim,Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Filamu Afrika kwa mwaka 2016 pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura(wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Grabriel(wa pili kushoto), kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso na kushoto ni  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
--
Na: Immaculate Makilika MAELEZO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  amesema Serikali imefarijaka kwa ushindi wa wasanii wa filamu nchini walioshinda tuzo za  filamu Afrika za mwaka 2016(African Magic Viewers Choice Award) ziliyofanyika jijini Lagos nchini Nigeria mwishoni wa wiki iliyopita.

Waziri Mkuu Majaliwa, amesema hayo leo katika ukumbi wa mikutano ulipo katika  Ofisi yake Jijini Dares Salaam, alipokutana na washindi wa tuzo za  filamu Afrika za mwaka 2016 (AMVCA)  ambao ni  Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki na Single  Mtambalike ‘Richie’ aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili pamoja Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Annastazia Wambura,Katibu Mkuu wa wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso na wasanii wa filamu.

 “Serikali imefarijika sana kwa nyie kwenda Nigeria na kushinda na mmetumia lugha ya Kiswahili, lazima tutumie nafasi hii kuwatangaza  pia  mmuendelee na fani hii ili kuvutia wengi zaidi” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewapongeza wasanii hao na kusema kuwa  Serikali itaendelea kushirikiana  na wasanii wakati wowote na amewataka kujipanga vizuri kutumia vyama vyao vya sanaa na kusisitiza kuwa  Mhe.  Rais John Pombe Magufuli ametoa matamko kadhaa kuhusu sanaa  na wasanii  na ameendelea kushughulikia malalamiko yao ikiwemo suala la COSOTA, na kusema kuwa  baada ya taratibu zote kukamilika  suala hilo litasimamiwa na Wizara inayohusika na kazi za Sanaa.

Waziri Mkuu Majaliwa, pia amewataka watanzania kuacha tabia ya kutojiamini  na kujidharau, na kuwataka watu waige mfano kwa wasanii hao, na kuwashauri wasanii wote kwa ujumla kutumia vyombo vya habari kujiimarisha na kujitangaza.

Kwa  upande wao, wasanii waliopata  tuzo hizo kwa filamu ya “mapenzi ya Mungu” ya Elizabeth Michael na filamu ya “Kitendawili” ya Single  Mtambalike, wameishukuru Serikali kwa kuwathamini na kuonesha  ushirikiano katika kazi zao za sanaa, na wameahidi kuendelea kutengeneza  kazi nzuri za sanaa ili ziweze kuitangaza Tanzania kimataifa.
Naye, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Saimon Mwakifamba ameishukuru Serikali kwa jitihada mbalimbali  inazofanya katika kusaidia tasnia ya sanaa kwa ujumla na ameahidi kuendelea kushirikiana na  Serikali katika kuendeleza tasnia hiyo kimataifa.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: SERIKALI YAFARIJIKA KWA USHINDI WASANII WA TUZO ZA FILAMU
SERIKALI YAFARIJIKA KWA USHINDI WASANII WA TUZO ZA FILAMU
https://3.bp.blogspot.com/-OIZTp_sjXLQ/VuLbIxRT9vI/AAAAAAADf1M/na4lKKesac0eXUTdt1JY2NFcQA5t5B5JA/s640/lul1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-OIZTp_sjXLQ/VuLbIxRT9vI/AAAAAAADf1M/na4lKKesac0eXUTdt1JY2NFcQA5t5B5JA/s72-c/lul1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/serikali-yafarijika-kwa-ushindi-wasanii.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/serikali-yafarijika-kwa-ushindi-wasanii.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago