Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Rais wa Vietnam atembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA)

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Adelm Meru kwa Rais wa Vietnam, Mhe....


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Adelm Meru kwa Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara baada ya Rais huyo kuwasili Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa ajili ya kutembelea Mamlaka hiyo la uwekezaji na kujionea shughuli zinazofanywa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulishaMkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mhe. Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mwijage akimwelezea  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong shughuli zinazofanywa na Kampuni ya Simu ya Halotel kutoka nchini Vietnam, ambapo alimwonyesha Vocha za muda wa maongezi za mtandao huo ambazo zinapatikana katika gharama tofauti kulingana na nafasi ya kifedha ya mtumiaji.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong akiongea na viongozi wa Serikali ya Tanzani na Vietnam pamoja na wafanyabiashara katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa Ofisi za EPZA. Mhe. Truong alieleza kuwa Serikali ya Tanzania ijiandae kupokea wawekezaji wengi zaidi wa Kampuni ya Halotel kutoka nchini kwake kupitia fursa za uwekezaji zilizopo katika kituo cha Uwekezaji cha EPZA .

Mhe. Mwijage akiwasilisha taarifa ya Wizara juu ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania, hali halisi ya uwekezaji katika kituo cha EPZA na  jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuanzisha maeneo ya uwekezaji katika mikoa yote nchini kufuatia shughuli za kiuchumi zinazofaa katika Mkoa husika.

Mkurugenzi wa EPZA Kanali Mstaafu Mhe. Joseph Simbakalia akieleza hali ya uwekezaji katika kituo hicho ambacho kimegawanya maeneo ya uwekezaji katika kanda mbili, ambapo alisema kuna maeneo ya uwekezaji ya Serikali na binafsi pamoja na mikakati ya kuongeza  kanda nyingine za uwekezaji  sambamba na taarifa ya usimamizi wa kanda zilizopo.

Mkuruzenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki kulia akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Balozi Abdulrahman Shimbo anayewakilisha pia nchini Vietnam wakifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea.

Sehemu ya Maafisa wa EPZA waliohudhuria Mkutano wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka kwa viongozi

Sehemu ya Maafisa Waandamizi kutoka Vietnam na Tanzania wakiwa EPZA
Mhe. Mwijage akimkabidhi zawadi ya kinyago Mhe. Truong Tan Sang

Mhe. Truong naye alikabidhi zawadi ya picha ya maua kwa Mhe. Waziri ambapo alieleza ni maua yanayopendwa nchini Vietnam

Wakijadili jambo mara baada ya kumaliza Mkutano katika ofisi za EPZA Makao Makuu, Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Rais wa Vietnam atembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA)
Rais wa Vietnam atembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA)
https://3.bp.blogspot.com/-dmpgdZREQL0/VuFWJJm7o1I/AAAAAAAAnUA/EsuRMzyhJ3o/s640/719A7061.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-dmpgdZREQL0/VuFWJJm7o1I/AAAAAAAAnUA/EsuRMzyhJ3o/s72-c/719A7061.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/rais-wa-vietnam-atembelea-mamlaka-ya.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/rais-wa-vietnam-atembelea-mamlaka-ya.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago