Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwakiklishi Maalum wa Umoja wa Afrika kwa Libya Akutana na Waziri wa Nchi wa UAE Mheshimiwa Reem Ebrahim Al-Hashimy, Dubai, UAE

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika Utatuzi wa Mgogoro wa Libya akwa katika mazungumz...

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika Utatuzi wa Mgogoro wa Libya akwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mheshimiwa Reem Ebrahim  Al-Hashimy alipomtembelea katika ofisi yake jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
----
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika Utatuzi wa Mgogoro wa Libya amekutana na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mheshimiwa Reem Ebrahim  Al-Hashimy alipomtembelea katika ofisi yake jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Rais Mstaafu Kikwete aliyewasili Dubai akitokea Tunisia kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi Majirani wa Libya amefanya mazungumzo hayo leo yenye lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa wa Libya. Mkutano huo ni muendelezo wa utekelezaji wa hadidu za rejea za AU zinazomtaka Mwakilishi Maalum kukutana na wadau wote wa Libya kwa  lengo la kutafuta majawabu ya kudumu ya mgogoro huo. Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ni moja ya nchi zinazoshiriki katika utafutaji wa utatuzo wa mgogoro huo na mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab Legue).

Katika mazungumzo hayo, Mwakilishi Maalum wa AU amemuelezea  Waziri Reem mtazamo na dhamira ya AU katika kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya. Amemjulisha jitihada ambazo amechukua toka kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo ikiwemo kukutana na viongozi wa Serikali ya Muafaka wa Kitaifa ya Libya,wadau wa siasa wa ndani ya Libya na wadau  wengine wa siasa wa ndani na nje ya Libya. Amemuelezea pia utayari wa AU kushirikiana na UAE na wadau wengine ili kuwa na sauti moja ya kushawishi pande zote za mgogoro wa Libya kuheshimu na kutekeleza Makubaliano ya Kisiasa ya Libya (Libya Political Agreement) yaliyosainiwa tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco.  Makubaliano hayo yanahusisha pamoja na mambo mengine Bunge kuidhinisha muundo wa Baraza la Mawaziri na kuhamishia shughuli za Serikali makao makuu ya nchi hiyo jijini Tripoli.

Kwa upande wake, Waziri Reem amempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa kwake kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro huo. Amemuelezea Rais Mstaafu Kikwete kuwa ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa wa uongozi na utatuzi wa migogoro barani Afrika. Amemueleza kuwa UAE ingependa kuona mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi haraka ili kurejesha hali ya usalama na kuwaondolea madhila wananchi wa Libya hususan wanawake na watoto. Amemhakikishia ushirikiano wake binafsi na wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu katika kufanikisha wajibu wake huo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwakiklishi Maalum wa Umoja wa Afrika kwa Libya Akutana na Waziri wa Nchi wa UAE Mheshimiwa Reem Ebrahim Al-Hashimy, Dubai, UAE
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwakiklishi Maalum wa Umoja wa Afrika kwa Libya Akutana na Waziri wa Nchi wa UAE Mheshimiwa Reem Ebrahim Al-Hashimy, Dubai, UAE
https://1.bp.blogspot.com/-ZErWnia6_uo/VvUbwrF5zII/AAAAAAADgXs/X4Zh5AXeQS8hMxICisvu2-FAKG9tIx_zg/s640/Rais%2BMstaafu%2Bna%2BMwakiklishi%2BMaalum%2Bwa%2BUmoja%2Bwa%2BAfrika%2Bkatika%2Busuluhishi%2Bwa%2Bmgogoro%2Bwa%2BLibya%2Bakibadilishana%2Bmawazo%2Bna%2BWaziri%2Bwa%2BNchi%2Bwa%2BUAE%2BMheshimiwa%2BReem%2BEbrahim%2BAl-Hashimy%2Bwalipokutana%2Bofisini%2Bkwake%2Bjana.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-ZErWnia6_uo/VvUbwrF5zII/AAAAAAADgXs/X4Zh5AXeQS8hMxICisvu2-FAKG9tIx_zg/s72-c/Rais%2BMstaafu%2Bna%2BMwakiklishi%2BMaalum%2Bwa%2BUmoja%2Bwa%2BAfrika%2Bkatika%2Busuluhishi%2Bwa%2Bmgogoro%2Bwa%2BLibya%2Bakibadilishana%2Bmawazo%2Bna%2BWaziri%2Bwa%2BNchi%2Bwa%2BUAE%2BMheshimiwa%2BReem%2BEbrahim%2BAl-Hashimy%2Bwalipokutana%2Bofisini%2Bkwake%2Bjana.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-na_25.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-na_25.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago