Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kwenye mgogoro wa Libya ashiriki Kikao cha Kamati ya Uandishi wa Bunge la Katiba ya Libya

Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ame...

Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa  Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.

Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu. Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao

 Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote. 

Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco. Amehimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League)  na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kwenye mgogoro wa Libya ashiriki Kikao cha Kamati ya Uandishi wa Bunge la Katiba ya Libya
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kwenye mgogoro wa Libya ashiriki Kikao cha Kamati ya Uandishi wa Bunge la Katiba ya Libya
https://1.bp.blogspot.com/-5n0QOS4odZQ/Vu7v5BElz8I/AAAAAAADgJM/ujAe42T3mls-PNYecVhXVk2ifoaa-VvPQ/s640/Rais%2BMstaafu%2BJakaya%2BKikwete%2Bna%2BMwakilshi%2Bwa%2BUmoja%2Bwa%2BAfrika%2Bakitoa%2Bhotuba%2Byake%2Bya%2Bufunguzi%2B%2Bwa%2BMkutano%2Bwa%2BKamati%2Bya%2BUandishi%2Bwa%2BKatiba%2B%2528Libyan%2BConstitution%2BDrafting%2BCommittee%2529.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-5n0QOS4odZQ/Vu7v5BElz8I/AAAAAAADgJM/ujAe42T3mls-PNYecVhXVk2ifoaa-VvPQ/s72-c/Rais%2BMstaafu%2BJakaya%2BKikwete%2Bna%2BMwakilshi%2Bwa%2BUmoja%2Bwa%2BAfrika%2Bakitoa%2Bhotuba%2Byake%2Bya%2Bufunguzi%2B%2Bwa%2BMkutano%2Bwa%2BKamati%2Bya%2BUandishi%2Bwa%2BKatiba%2B%2528Libyan%2BConstitution%2BDrafting%2BCommittee%2529.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-na.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-na.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago