Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora, Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa kutatua kero ya maji

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora,  Seleman Jafo  --- NA VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI  NAIBU Waz... Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora,  Seleman Jafo
 ---
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI
 NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora,  Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa kutatua kero ya maji kwa muda mrefu.

 Jafo ambae pia ni mbunge wa jimbo la Kisarawe alisema, hawawezi kuendelea kukaa na watumishi ambao hawaguswi na matatizo ya wananchi.

 Alitoa agizo hilo juzi mjini Kisarawe, kwenye mkutano aliouandaa kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumpa ridhaa ya kuendelea kuongoza jimbo hilo, na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hao.

 Naibu Waziri huyo alimtaka Materu kuachia nafasi ya Meneja ili apangiwe kazi nyingine kwani ameshindwa kutatua changamoto ya maji katika mji wa Kisarawe.

 “Mkurugenzi mtafutie kazi nyingine katika ofisi yako, hatuwezi kuwa na watu ambao hawaguswi na matatizo ya watu tafuta atakayekaimu nafasi yake katika kipindi hiki.

 Hatufanyi mambo ya kuchekeana, na hatuwezi kuibadilisha  Kisarawe yetu kama tutaendelea kuwavumili watumishi wanaochangia kudumaza maendeleo”alisema Jafo.

 Inadaiwa kuwa, Materu amekua meneja wa Mamlaka hiyo kwa zaidi ya miaka kumi lakini hakuna njia mbadala iliyobuniwa na mamlaka hiyo kuondoa tatizo la maji kukosekana mara kwa mara.
 Mji huo wa Kisarawe una chanzo cha maji cha kimani ambacho kinatoa lita 16000 kwa saa na chanzo kingine cha minaki kinachotoa zaid ya lita 10,000 kwa saa hali ambayo ni dhahiri kusingekuwepo na tatizo la  maji.

 Wananchi waliohudhuria katika mkutano huo walifurahishwa na kitendo kilichofanywa na mbunge wao huku wakiendelea kumuomba ahamie katika idara ya ardhi.

 Mwajuma Yusuph, Salehe Ally na Said Issa walisema kitendo cha kuondolewa Meneja huyo kitaleta mabadiliko kwani baadhi ya watumishi wanafanya kazi kwa mazoea bila kujali adha inayowapata wananchi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora, Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa kutatua kero ya maji
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na Utawala bora, Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa kutatua kero ya maji
https://1.bp.blogspot.com/-DGbvDqls0rE/VtWStqLs8oI/AAAAAAADfZo/oU8EeE6iJbE/s640/selemani-Jaffo.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-DGbvDqls0rE/VtWStqLs8oI/AAAAAAADfZo/oU8EeE6iJbE/s72-c/selemani-Jaffo.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/naibu-waziri-ofisi-ya-rais-tamisemi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/naibu-waziri-ofisi-ya-rais-tamisemi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago