Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kushughulikiwa kwa wakati

 Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Grifin Mwakapeje akitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta...

 Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Grifin Mwakapeje akitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta ya Sheria kuendelea kutumia huduma ambazo zinazotolewa na Wizara hiyo ili kuwezesha kupata haki kwa wakati.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria  Bi Farida Khalfan (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo Pichani) kuhusu utaratibu wa Wizara katika kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko  Grifin Mwakapeje na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ufatiliaji Haki Bi Mary Mrutu.
----
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imedhamiria kuendelea kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayowasilishwa ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

aAidha , Mwakapeje amesema Wizara hiyo imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusu ucheleweshwaji wa utekelezaji wa amri mbali mbali zinazotolewa na mahakama,ucheleweshaji wa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri baada ya kumalizika mahakamani.

Malalamiko mengine yanahusu msongamano wa mahabusu, ucheleweshwaji wa upelelezi,wananchi kubambikiwa kesi,migogoro ya ardhi navitendo vya rushwa.

Akizungumzia wajibu wa  Wizara hiyo Mwakapeje amesema ni kuyaratibu na kuyawasilisha kwenye taasisi husika ili kupata muafaka wa malalamiko hayo kwa wakati.

Hatua nyingine inayochukuliwa na Wizara katika kuwasaidia wananchi kupata haki kwa wakati, ni kutoa msaada wa kisheria unapohitajika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo ili kuwawezesha wananchi kupata haki kwa wakati.

Katika kushughulikia malalamiko hayo “Serikali inayo dhamira ya dhati yakuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki kwa wakati.” Amesema Mwakapeje.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi Farida Khalfan akizungumzia Mfumo wa kupokea malalamiko amesema kuwa wananchi wanaweza kufika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo mtaa wa Sokoine au kuandika barua ili kuwasilisha malalamiko yao na yatafanyiwa kazi kwa wakati.

 Wizara ya Katiba na Sheria ina Dhamana ya Kusimamia masuala ya Katiba na Sheria ambapo inatoa huduma mbali mbali za kisheria kwa wananchi,mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kushughulikiwa kwa wakati
Malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kushughulikiwa kwa wakati
https://1.bp.blogspot.com/-kgDsjSYV5-A/VtmRxYrtmzI/AAAAAAADfmY/Hytg8adTeXc/s640/tai2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-kgDsjSYV5-A/VtmRxYrtmzI/AAAAAAADfmY/Hytg8adTeXc/s72-c/tai2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/malalamiko-yanayohusu-upatikanaji-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/malalamiko-yanayohusu-upatikanaji-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago