Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

DARAJA KIGAMBONI KUFUNGULIWA APRILI 16, MWAKA HUU.

  Mwonekano wa daraja la Kigamboni ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao.   Mwonekano wa lango la kuingilia daraja la Kigamboni kw...

  Mwonekano wa daraja la Kigamboni ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao.
  Mwonekano wa lango la kuingilia daraja la Kigamboni kwa upande wa Kigamboni, linavyoonekana pamoja na vyumba vya kukatia tiketi
  Mwonekano wa vyumba vya ofisi zitakazotumiwa na wasimamizi wa Daraja la Kigamboni.
 Barabara za maingilio (inter change) ya Daraja la Kigamboni upande wa Kurasini.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es salaam.
 Wazirib wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es salaam.
---
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja laKigamboni litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu.
Amesema kazi inayoendelea sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupimaubora wa daraja hilo ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.
 
Amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepukavitendo vya hujuma  ili lidumu kwa muda mrefu.
 
“Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka,hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa Mbarawa.
 
Amebainisha kuwa Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya
daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalamabarabarani wanapovuka katika daraja hilo.
 
Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalamwanaendelea na taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudukupitisha uzito uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.
 
Amesema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na
awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.
 
Takribani shilingi bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa
kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na Kigamboni.
 
 
IMETOLEWA NA 
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, 
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: DARAJA KIGAMBONI KUFUNGULIWA APRILI 16, MWAKA HUU.
DARAJA KIGAMBONI KUFUNGULIWA APRILI 16, MWAKA HUU.
https://1.bp.blogspot.com/-80f-mCDS7WU/VulfWxl-F-I/AAAAAAADf9g/AKDxzEn-1zMThltIO5jAuszZaOWi3_VxA/s640/20.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-80f-mCDS7WU/VulfWxl-F-I/AAAAAAADf9g/AKDxzEn-1zMThltIO5jAuszZaOWi3_VxA/s72-c/20.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/daraja-kigamboni-kufunguliwa-aprili-16.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/daraja-kigamboni-kufunguliwa-aprili-16.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago