Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Balozi wa Norway atembelea Mkoa wa Iringa

 Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Ka...

 Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa shule hiyo.
 Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad akiwa na Mwenyeji wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Shuleni hapo tayari kwa uzinduzi rasmi.
 Mtoto Anderson akifuahia jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
 Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, wakiangalia umahiri wa Mtoto Martha katika kutaja mikoa ya Tanzania aliyokuwa akiitaja kwa kuonyesha ramani.
watoto wa Sallirud Montesori Ilula wakiimba ​ 
---
 

​ Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, amefanya ziara ya siku 2 Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Kilolo na Wilaya ya Iringa na kufanya shughuli ya kuzindua shule ya watoto ya awali inayofundisha mwa mfumo wa Montesori.

Shule hiyo iliyopo Ilula, katika wilaya ya Kilolo inafadhiriwa na wanachi wa Norway kupitia kwa mdau wa Maendeleo Norway na familia yake Bw. Osmund pamoja na wananchi wengine ambao wameunda NGO iitwayo Ilula Orphanage Program (IOP) chini ya Mwenyekiti wake raia wa Marekeni Bibi Berit Skaare.

Akimkaribisha Balozi kuzindua Shule hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, alisifu na kushukuru wananchi wa Norway kwa kazi kubwa wanayofanya Tanzania hasa katika elimu, Pia alipongeza juhudi za wananchi wa Norway wanavyo jali watanzania.

Kasesela aliagiza Halmashauri kutunza kituo hicho na kuhakikisha kinaendelea kuwa bora na kufundisha watoto wetu, Pia aliagiza Halmashauri iangalie uwezekano wa kutengeneza barabara ya kufika kituoni hapo kwani kwa sasa hairidhishi. 

Nae Balozi wa Norway nchini, Hanne Marie, alishukuru serikali ya Tanzania na kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kasi anayokwenda nayo kukomboa elimu. Pia alishukuru Mkoa wa Iringa kwa kutoa ardhi ili ijengwe shule hiyo ya kisasa. Balozi aliaahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja ya elimu hasa elimu ya ufundi stadi.

Balozi aliendelea na ziara yake kukagua miradi ya REA ambayo baadhi inafadhiliwa na serikali ya Norway. Atatembelea mradi wa Mgama ulioko kata ya Lumuli Iringa.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Balozi wa Norway atembelea Mkoa wa Iringa
Balozi wa Norway atembelea Mkoa wa Iringa
https://3.bp.blogspot.com/-h3Ctq5PR0gE/VtmNfCgNJTI/AAAAAAADfmA/gBkZrUN97xM/s640/IMG_7310.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-h3Ctq5PR0gE/VtmNfCgNJTI/AAAAAAADfmA/gBkZrUN97xM/s72-c/IMG_7310.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/03/balozi-wa-norway-atembelea-mkoa-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/03/balozi-wa-norway-atembelea-mkoa-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago