Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu apokea vifaa katika wodi ya Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Muhimbili

 Baadhi ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mfanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa ya taifa (MSD) walishusha baadhi ya magodoro n...

 Baadhi ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mfanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa ya taifa (MSD) walishusha baadhi ya magodoro na vitanda vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisaidia kufagia,leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akisaidiana na mmoja  wa kijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kubeba boksi lenye takataka kwenda kuyatupa sehemu husika  wakati wakifanya usafi katika jengo ambalo liliamriwa na Mhe Rais liwe wodi ya  Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akipokea vifaa kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa yaTaifa Lauren Rugambwa Bwanakunu vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Muhimbili Prof Lawerence Mseru na nayefata ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya .
 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akielekezwa jambo katika nyaraka na katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya katika Kitengo cha Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Zuhura Abubakari mmoja ya wagonjwa waliohamishiwa kwenye wodi mpya ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 Wagonjwa wakiwa katika wodi ya wazazi .
Mafundi wakifunga vitanda katika wodi mpya ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Wagonjwa wakiwa katika wodi ya wazazi .(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii na
Raymond Mushumbusi MAELEZO.
---
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amepokea vifaa vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni agizo la Mhe.Rais alililolitoa mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika kuhakikisha kuwa wakinamama wanaojifungua hawalali chini.

Akipokea vifaa hivyo Mhe. Ummy Mwalimu amesema anamshukuru sana Mhe Rais kwa kuona changamoto hii ya wakina mama kulala chini wakati wakitoka kujifungua na kumuahidi Mhe. Rais kusilimamia vyema suala hilo na kuwaagiza wakurugenzi husika kumpa taarifa ya kuhusu vitanda na magodoro katika Hospitali zote zilizo chini ya wizara yake.

“ Kuanzia sasa sitolala na natuma salamu kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa fursa hii ni wajibu wao kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya afaya hasa katika vifaa hususan vitanda na magodoro ili kupunguza tatizo hili la wagonjwa katika Hospitali zetu kulala chini wakati tuna uwezo wa kupata vitanda na magodoro”

‘”Mhe.Rais amenifundisha na ametufundisha sote kwamba kutatua jambo sio mpaka mkae vikao au semina ili kujadili ila inawezekana kama mkiweka nia ya kulifanya jambo hilo na kuachana na zile kauli za tunalifanyia kazi, tupo katika michakato na kauli kama hizo zisizotatua tatizo kwa wakati unaotakiwa”alisema Ummy.

Bohari ya Dawa ya Taifa imekabidhi jumla ya vitanda 120, Magodoro 120, Mashuka 480, vitanda vya kuzalishia 10,vitanda 10 vya kulaza watoto ambao hawajatimia Njiti na jumla ya vifaa vyote vina thamani ya shilling Million 100.

Uaandaaji wa wodi hiyo ya akimama wanaojifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umekuja baada ya agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa hivi karibuni alipokuwa akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es Salam na kutoa siku mbili kwa wizara Ya Afya kuhamisha ofisi zilizokuwepo za kitengo Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto na kuifanya kuwa wodi ya akina mama ili kupunguza tatizo la kulala chini kwa akina mama wanaotoka kujifungua.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu apokea vifaa katika wodi ya Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Muhimbili
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu apokea vifaa katika wodi ya Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Muhimbili
https://1.bp.blogspot.com/-GlVpffgpIK8/VsH2jSzBHII/AAAAAAADe98/SvvJwchXhmo/s640/U5.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-GlVpffgpIK8/VsH2jSzBHII/AAAAAAADe98/SvvJwchXhmo/s72-c/U5.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/waziri-wa-afya-maendeleo-ya-jamiijinsia.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/waziri-wa-afya-maendeleo-ya-jamiijinsia.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago