Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WANACHACHAMA WA CCM MKOANI MWANZA WAONYA VITEGA UCHUMI VYA CHAMA KUTUMIKA VIBAYA.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameonya juu ya baadhi ya Wawekezaji nchini wan...


Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameonya juu ya baadhi ya Wawekezaji nchini wanaotumia Vitega uchumi vya chama hicho bila kufuata mikataba wanayopewa.
--
Wanachama hao walitoa kauli hiyo wiki hii baada ya Wawekezaji wanaotumia majengo ya CCM Kata ya Kirumba, kudaiwa kukiuka masharti yao na hivyo kutumia majengo hayo bila kuyalipia kodi ya pango kwa muda mrefu.

Ni kutokana na hatua hiyo, Wanachama hao walichukua maamuzi ya kufunga Majengo hayo ambayo yanatumiwa na Tasisi ya Mikopo ya Wadoki pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, huku taratibu nyingine za kisheria zikiendelea, lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba watumiaji wa majengo hayo wanayalipia kodivwanayodaiwa vinginevyo watafurushwa nje ya majengo hayo.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Abubakary Francis Kweyamba alithibitisha kwamba wanachama hao wamefikia maamuzi hayo, kutokana na kutumia majengo ya chama katika kata hiyo huku wakiwa hawayalipii kodi na hivyo kukisababishia chama usumbufu mkubwa wa kuendesha shughuli zake za kiofisi huku akisisitiza msimamo wa kuendelea kuyafunga majengo hayo.

Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, walisema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na wanachama hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi ngazi ya Mkoa ya Chama hicho na kuonekana kwamba wawekezaji hao hawatii makubaliano yaliyofikiwa.

Suala hilo lilifikishwa katika Kituo cha Polisi Kirumba na kila upande umetakiwa kuwasilisha vielelezo vyake ili kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa upangaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Meneja wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba mzungumzaji ni Mkurugenzi wake ambae alisema amesafiri huku Uongozi wa Wadoki Saccos ukishindwa kupatikana.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WANACHACHAMA WA CCM MKOANI MWANZA WAONYA VITEGA UCHUMI VYA CHAMA KUTUMIKA VIBAYA.
WANACHACHAMA WA CCM MKOANI MWANZA WAONYA VITEGA UCHUMI VYA CHAMA KUTUMIKA VIBAYA.
https://1.bp.blogspot.com/-uXdjrNJNtbk/VsQQuGWdCMI/AAAAAAAAJa0/JFRLx9FpOdQ/s640/CCM.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-uXdjrNJNtbk/VsQQuGWdCMI/AAAAAAAAJa0/JFRLx9FpOdQ/s72-c/CCM.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/wanachachama-wa-ccm-mkoani-mwanza.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/wanachachama-wa-ccm-mkoani-mwanza.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago