Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TTCL yakanusha mfumo wake wa mawasiliano kuingiliwa

Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuka...

Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kukanusha taarifa za kampuni hiyo kudukuliwa. Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kukanusha taarifa za kampuni hiyo kudukuliwa.Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kukanusha taarifa za kampuni hiyo kudukuliwa. Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kukanusha taarifa za kampuni hiyo kudukuliwa.Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka akifafanua jambo kwenye mkutano na vyombo vya habari leo. Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka akifafanua jambo kwenye mkutano na vyombo vya habari leoBaadhi ya wanahabari katika mkutano leo na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Baadhi ya wanahabari katika mkutano leo na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
---
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo umeingiliwa na wadukuzi. Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Nicodemus Thomas Mushi alisema taarifa zinazotolewa si za kweli hivyo kuwataka wateja wao wazipuuze.

 “...Tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote,” alisema Thomas Mushi. Aidha, tunapenda kuwathibitishia kuwa, taarifa za Wateja wetu wote ikiwemo Serikali , Idara, Wakala na Taasisi za Umma, Taasisi za fedha, Mashirika, Makampuni na Watu binafsi zipo salama kabisa. 

Ukweli huu unathibitishwa na Wateja wao pia kwani hadi sasa, hakuna hata mmoja aliyeleta taarifa za kukosa huduma ama kupata athari zozote kutokana na tetesi hizo. Hata hivyo, alisema pamoja na taarifa hizo, Wataalamu wa kampuni hiyo wanaendelea kuwa macho kwa muda wote, ili kuhakikisha kuwa, wanafanyia kazi kila taarifa ama tishio la kiusalama linaloweza kujitokeza katika mfumo wao. “TTCL inaendelea kuwaomba Umma na Wateja wetu wote kuendelea na majukumu yao kama kawaida bila wasiwasi wowote. TCCL inawaleta Karibu.

” Alisema Thomas Mushi. Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka alisema kitengo chao baada ya tetesi hizo kimefanya uchunguzi wa kina na hakuna ashirio lolote la mifumo yao kuingiliwa (kudukuliwa) kama ilivyoelezwa. Alisema kitengo hicho kina wataalam ambao muda wote wapo kazini kufuatilia ufanisi wa mfumo wa mawasiliano wa kampuni yao hivyo kuwaondoa hofu wateja wao. 


 “... Baada ya taarifa hizo Kitengo cha Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano ya Kampuni ya TTCL kiliingia kazini ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na kufanya majaribio ya kitaalamu ili kuthibitisha usalama wa mifumo yetu. Baada ya utafiti wa kina na majaribio ya kitaalamu, tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi...” alisema.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TTCL yakanusha mfumo wake wa mawasiliano kuingiliwa
TTCL yakanusha mfumo wake wa mawasiliano kuingiliwa
http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/02/IMG_0142.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/ttcl-yakanusha-mfumo-wake-wa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/ttcl-yakanusha-mfumo-wake-wa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago