Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TAARIFA YA UFAFANUZI KWA UMMA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA CHINI KUHUSU ADHABU YA KIFUNGO CHA NJE KWA MUJIBU WA SHERIA YA HUDUMA KWA JAMII

  Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza)   Kwa mujibu wa kifungu na 3(2) (a) cha Sh...


 Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,Afisa Habari wa Jeshi la Magereza)


 
Kwa mujibu wa kifungu na 3(2) (a) cha Sheria ya Huduma kwa Jamii ya mwaka 2002 kifungo cha nje ni utaratibu ambao unampa fursa mfungwa kutumikia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli/kazi zisizo na malipo kwa manufaa ya jamii.
Utaratibu huu hutolewa kwa wafungwa ambao vifungo vyao havizidi miaka mitatu bila kujali wana faini au hawana. Wapo wahalifu wanaohukumiwa moja kwa moja mahakamani kwenda kutumikia kifungo cha nje na wengine huingia gerezani kwanza na baadaye utaratibu wa maombi maalum hufanyika ili mfungwa husika kwenda kutumikia kifungo kwa utaratibu huo.
Sheria ya Magereza Sura ya 58 kifungu Na. 52 (1) (2) inatoa utaratibu wa kumuondoa mfungwa aliyepo gerezani huku akiwa ana sifa ya kutumikia kifungo chake kwa utaratibu wa huduma kwa jamii.
Kifungu hicho cha Sheria kinaeleza kuwa pale ambapo Mkuu wa gereza atajiridhisha kuwa kuna mfungwa ambaye ana sifa ya kutumikia kifungo chake chini ya utaratibu wa huduma kwa jamii, atamshauri mfungwa huyo juu ya utaratibu huo kwa kuzingatia sifa alizonazo na ikiwa mfungwa huyo ataridhia kuachiliwa kwake katika utaratibu wa huduma kwa jamii, Mkuu wa Gereza atawasilisha maombi maalum katika Mahakama iliyomfunga kwa ajili ya maandalizi ya kuachiliwa kwa mfungwa huyo katika utaratibu wa huduma kwa jamii.
Mahakama baada ya kupokea maombi hayo, itafanya uchunguzi kulingana na kifungu Namba 3 cha Sheria ya Huduma kwa jamii na ikijiridhisha kuwa mfungwa husika ana sifa za kutumikia katika utaratibu wa Huduma kwa jamii, Mahakama husika itatoa amri ya kuachiliwa kwa mfungwa huyo chini ya utaratibu huo.
Aidha, Usimamizi na Utekelezaji wa adhabu hii husimamiwa na Idara inayojitegemea ya Huduma kwa Jamii iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mfungwa anayetumikia kifungo cha nje ni lazima aishi kwa kufuata Sheria na masharti aliyopangiwa. Masharti hayo ni kuwa chini ya uangalizi maalum, kutoondoka nje ya Mkoa bila kibali na kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka muda wake wa kifungo chake utakapokamilika.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
09 Februari, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TAARIFA YA UFAFANUZI KWA UMMA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA CHINI KUHUSU ADHABU YA KIFUNGO CHA NJE KWA MUJIBU WA SHERIA YA HUDUMA KWA JAMII
TAARIFA YA UFAFANUZI KWA UMMA KUTOKA JESHI LA MAGEREZA CHINI KUHUSU ADHABU YA KIFUNGO CHA NJE KWA MUJIBU WA SHERIA YA HUDUMA KWA JAMII
https://3.bp.blogspot.com/-lJ0b5Jdof5s/Vrn772HiExI/AAAAAAADeyY/_0SyL0yK9pI/s640/MBJ1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-lJ0b5Jdof5s/Vrn772HiExI/AAAAAAADeyY/_0SyL0yK9pI/s72-c/MBJ1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/taarifa-ya-ufafanuzi-kwa-umma-kutoka.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/taarifa-ya-ufafanuzi-kwa-umma-kutoka.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago