Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa ya IKULU:Rais Dr John Magufuli ampa pole mke wa Waziri mkuu Mstaafu mama Tunu Pinda

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda -- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu z...

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.

Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.

“Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku” alisema Rais Magufuli.

Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09 Februari, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa ya IKULU:Rais Dr John Magufuli ampa pole mke wa Waziri mkuu Mstaafu mama Tunu Pinda
Taarifa ya IKULU:Rais Dr John Magufuli ampa pole mke wa Waziri mkuu Mstaafu mama Tunu Pinda
https://2.bp.blogspot.com/-36jOzCb2Kvc/VroBLKyRf0I/AAAAAAADezM/sbI27LfSyGA/s640/pinda001bc.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-36jOzCb2Kvc/VroBLKyRf0I/AAAAAAADezM/sbI27LfSyGA/s72-c/pinda001bc.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/taarifa-ya-ikulurais-dr-john-magufuli_9.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/taarifa-ya-ikulurais-dr-john-magufuli_9.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago