Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Serikali yabaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 ATCL,Yamsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa  ---- Na Lorietha Laurence-Maelezo Serikali imebaini wizi wa  t...

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa 
----
Na Lorietha Laurence-Maelezo

Serikali imebaini wizi wa  takribani  shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa  wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali  imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi  cha polisi  kitengo cha usalama mtandaoni  ili kubaini mtandao mzima uliohusika  ” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa  shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya  kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.
“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

 Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa  njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Serikali yabaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 ATCL,Yamsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi
Serikali yabaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 ATCL,Yamsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi
https://3.bp.blogspot.com/-5rrY5ekefhY/Vrs7purY2fI/AAAAAAADez8/AgqOP2HPZDQ/s640/Makame_Mbarawa_IAEA.png
https://3.bp.blogspot.com/-5rrY5ekefhY/Vrs7purY2fI/AAAAAAADez8/AgqOP2HPZDQ/s72-c/Makame_Mbarawa_IAEA.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/serikali-yabaini-wizi-wa-takribani.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/serikali-yabaini-wizi-wa-takribani.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago