Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Serikali yaagiza vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya watu wenyeUlemavu

 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(HawapoPichani) kuh...

 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(HawapoPichani) kuhusu vyombo vya habari kutekeleza Sheria ya Watu wenye Ulemavu katika kupata habari.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi (Aliyekaa) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa kikao chake na vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini  Dar es Salaam. Picha zote na Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
---
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (WatuwenyeUlemavu) Dkt  Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuzingatia Sheria ya Watu wenye ulemavu kwa kuhabarisha kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kutoa habari,

Akitoa agizo hilo mbele ya vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuwakumbuka na watu wenye ulemavu katika utoaji wa taarifa mbalimbali katika Magazeti, Radio naTelevisheni hasa kwa kuzingatia lugha za alama ambazo zitawawezesha kuelewa habari husika.

“ Naomba tubadilike wanahabari kwa kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuwahabarisha na wao pia, nawataka wamiliki wa vyombo vya habari hususan Televisheni kuweka lugha za alama kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupata habari mbalimbali zinazojiri katika taifa”

“Vyombo vya habari vinatakiwa kubadili uono wao juu ya walemavu na sio kwa kuangalia mambo hasi tu yahusiyo walemavu kwamba wana shinda,hawawezi, wanahitaji msaada ila pia kwakuangalia mafanikio yao katika kuleta maendeleo ya taifa kiujumla” Alisema Dkt Possi.

Aidha Dkt Abdallah Possi amewataka waandishi wa habari hasa wa magazeti kuzingatia lugha wanazotumia  kandika habari za watu wenye ulemavu ili kuondoa fikra na dhana hasi na unyayapaa juu ya walemavu huku akitolea mfano baadhi ya lugha zinazotumika na baadhi ya waandishi katika kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu kuwa hazistahili.

Ametaja mfano wa lugha ambazo sio sahihi katika uandishi wa habari za wenye ulemavu mfano maneno vipofu, viziwi,vilema na maneno mengine bali wanatakiwa kutumia maneno yenye staa na yasiyoleta picha ya unyanyapaa na udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa na udhalilishaji wa watu wenye ulemavu.

Kupata habari ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria No 9 ya Mwaka 2010 inavitaka vyombo vya habari kuhabarisha watu bila kuwabagua watu wenye ulemavu, tuelewe kwamba pia watu wenye ulemavu wana haki ya kupata taarifa kama watu wengine.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Serikali yaagiza vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya watu wenyeUlemavu
Serikali yaagiza vyombo vya habari kuzingatia Sheria ya watu wenyeUlemavu
https://2.bp.blogspot.com/-xTWLaVBvk9I/VsSVkat_HbI/AAAAAAADfFc/MvP3-YGxaYQ/s640/PO1.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-xTWLaVBvk9I/VsSVkat_HbI/AAAAAAADfFc/MvP3-YGxaYQ/s72-c/PO1.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/serikali-yaagiza-vyombo-vya-habari.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/serikali-yaagiza-vyombo-vya-habari.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago