Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

OFISI YA TAKWIMU TAIFA YATOA TAARIFA KIPIMO KINACHOTUMIKA KUPIMA MABADILIKO YA BEI ZA BIDHA NA HUDUMA MBALIMBALI ZINAZO TUMIWA NA SAMPULI WAKILISHI YA KAYA BINAFSI NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) w...


Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokua akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei   Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira na Bei, Ruth Minja. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
--
Story Na; Frank Shija, MAELEZO
Matumizi ya kaya kwenye biadhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.ambapo kwa ujumla wake mfumuko wa Bei umepungu
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.
 
 
“Matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007” Alisema Kwesigabo.
Aliongeza kuwa makundi mengi mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya matumizi ya kaya mwaka 2011/12 kuwa ni pamoja na Usafi asilimia 12.5 kutoka asilimia 9.5 mwaka 2007, Makazi Maji na Nishati asilimia 11.6 kutoka asilimia 9.2 mwaka 2007 na Mavazi na Viatu asilimia 8.3 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007.
Aidha kumekuwa na ongezeko la Zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007
Kwa upande wake Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi. Ruth Minja amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata Fahirisi za Bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katikia bidhaa na huduma muhimu ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri ,Maji na Nishati.
Aliongeza kuwa ili kupata matokeo ya mfumuko wa Bei kumekuwa na mtindo wa kufanya marejeo baada ya kila miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika mwaka 2007 na kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa za vyakula zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na usafiri asilimia 9.5 huku matumizi madogo zaidi yalikuwa ni huduma za afya kwa asilimia 0.9.
Takwimu hizi zimekuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na zimekuwa zikisaidia katika kupima na kuboresha sera za kifedha na mipango ya kiuchumi ya kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la Taifa,kuboresha mishahara ya wafanyakazi na mafao ya wafanyakazi waliostaafu.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: OFISI YA TAKWIMU TAIFA YATOA TAARIFA KIPIMO KINACHOTUMIKA KUPIMA MABADILIKO YA BEI ZA BIDHA NA HUDUMA MBALIMBALI ZINAZO TUMIWA NA SAMPULI WAKILISHI YA KAYA BINAFSI NCHINI TANZANIA
OFISI YA TAKWIMU TAIFA YATOA TAARIFA KIPIMO KINACHOTUMIKA KUPIMA MABADILIKO YA BEI ZA BIDHA NA HUDUMA MBALIMBALI ZINAZO TUMIWA NA SAMPULI WAKILISHI YA KAYA BINAFSI NCHINI TANZANIA
https://4.bp.blogspot.com/-RwRu4zQzoaI/Vrih6pCIDzI/AAAAAAAAVFU/KAJ3W-NN860/s640/_DSC0776.JPG
https://4.bp.blogspot.com/-RwRu4zQzoaI/Vrih6pCIDzI/AAAAAAAAVFU/KAJ3W-NN860/s72-c/_DSC0776.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/ofisi-ya-takwimu-taifa-yatoa-taarifa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/ofisi-ya-takwimu-taifa-yatoa-taarifa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago