Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

MWENYEKITI WA BODABODA MKOANI MWANZA ATOA TAHADHARI JUU YA VITENDO VYA UKWAPUAJI JIJINI MWANZA.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda (pichani), amewataharisha wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa makini...


Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda (pichani), amewataharisha wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa makini wawapo barabarani, ili kuepukana na vitendo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu kwa kutumia pikipiki.

Kayanda alitoa tahadhari hiyo jana Jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya ukwapuaji vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya waendesha pikipiki, jambo linalochafua taswira ya waendesha pikipiki Mkoani Mwanza.

Tayari watu kadha wamefikisha malalamiko yao kwa uongozi wa bodaboda Mkoani Mwanza, baada ya kukumbwa na kadhia ya kukwapuliwa mikoba pamoja na mabegi yao, ambapo mmoja wa wahanga wa matukio hayo Diana Abdallah ameeleza kukwapuliwa mkoba wake uliokuwa na pesa pamoja na vito vya thamani wakati akitokwa kwenye shughuli zake.

"Nilikuwa maeneo ya Nyegezi ambapo nilikuwa nikitoka kwenye shughuli zangu, nilikwapuliwa mkoba wangu ambao ulikuwa na pesa shilingi Laki Nane, Simu ya shilingi Laki mbili na nusu, Pete sita za Silver zenye thamani ya shili laki moja na elfu ishiri na sita pamoja na miwani ya macho ya shilingi Laki nne. Watuhumiwa waliweza kukamatwa na kesi iko polisi katika kituo cha Igogo".Alisema Abdallah

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu nchini Edwin Soko, analaani Vitendo hivyo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi ya watu kwa kutumia bodaboda ambavyo vimekuwa vikiwakumba watembea kwa miguu Jijini Mwanza, ambapo ameomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano wake kwa ajili ya kuvikomesha.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: MWENYEKITI WA BODABODA MKOANI MWANZA ATOA TAHADHARI JUU YA VITENDO VYA UKWAPUAJI JIJINI MWANZA.
MWENYEKITI WA BODABODA MKOANI MWANZA ATOA TAHADHARI JUU YA VITENDO VYA UKWAPUAJI JIJINI MWANZA.
https://3.bp.blogspot.com/-QKNu7jhr1ho/VsQIncelWCI/AAAAAAAAJak/B855s1Vcvbw/s640/IMG_4473.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-QKNu7jhr1ho/VsQIncelWCI/AAAAAAAAJak/B855s1Vcvbw/s72-c/IMG_4473.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/mwenyekiti-wa-bodaboda-mkoani-mwanza.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/mwenyekiti-wa-bodaboda-mkoani-mwanza.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago