Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda na wenzake watatu akiwemo dereva wa gari wamenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kupinduka

 Gari STK 9442 alilokua akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda likiw...

 Gari STK 9442 alilokua akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali hii leo jioni eneo la Mkundi mkoani Morogoro.
MKE wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda  na wenzake watatu akiwemo dereva wa gari wamenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kupinduka kutokana na kumgonga mwendesha bodaboda eneo la Mkundi Manispaa ya Morogoro katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea saa nane mchana leo katika eneo hilo wakati gari lenye namba za usajili STK 9442 aina ya Toyota Land Cruiser lilipomgonga mwendesha bodaboda akiwa na pikipiki yenye namba MC 647 BBA na kupinduka.
Mke huyo wa Waziri Mkuu mstaafu na wenzake watatu walijeruhiwa na walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kupatiwa matibabu na kuchunguzwa afya zao.  Mama Pinda na wenzake waliruhusiwa kuendelea na safari.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya alithibitisha kuwapokea majeruhi hao akiwemo Mama Tunu Pinda ambaye hakuumia sana licha ya kupata maumivu kifuani.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, mbali na Mama Tunu, majeruhi wengine ni dereva Angelo Mwisa (50), Gilbert Sampa (40) pamoja na mlinzi wa mke huyo wa Pinda, Gaudencia Tembo.
Alisema walipata majeraha madogo madogo kwenye mbavu na kifuani na baaada ya kupata matibabu wameruhusiwa kuendelea na safari ya kwenda Dar es Salaam. “Tumepokea majeruhi wanne akiwemo Mama Pinda hawakuumia sana, ni majeraha madogo ambapo dereva ameumia kidogo usoni na hali zao sio mbaya.
Jioni hii wanaendelea na safari, mikanda waliokuwa wamejifunga imesaidia kutopata majeraha makubwa,” alisema Dk Lyamuya. Alisema hospitali hiyo pia ilipokea mwili wa dereva wa bodaboda ambaye aligongwa katika eneo la tukio hilo na jina lake hadi jana lilikuwa halijatambuliwa.

Ajali hiyo ilitokana na mwendesha bodaboda aliyekatisha barabara kuu kutoka upande mmoja wa barabara kwenda mwingine bila kuchukua tahadhari na hivyo kusababisha kugongwa na gari hilo na kupinduka.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda na wenzake watatu akiwemo dereva wa gari wamenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kupinduka
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda na wenzake watatu akiwemo dereva wa gari wamenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kupinduka
https://4.bp.blogspot.com/-2tl626GVzxU/Vrn3wy0NOKI/AAAAAAADexw/5LwyGdnW374/s640/IMG_20160208_224021.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-2tl626GVzxU/Vrn3wy0NOKI/AAAAAAADexw/5LwyGdnW374/s72-c/IMG_20160208_224021.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/mke-wa-waziri-mkuu-mstaafu-tunu-pinda.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/mke-wa-waziri-mkuu-mstaafu-tunu-pinda.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago