Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

KIDOGO CHA UCHANGIAJI DAMU CHA MBAGALA RANGI TATU JIJINI DAR CHAZINDULIWA LEO.

Wananchi wakijitolea damu katika kituo cha Rangi tatu jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck ...

Wananchi wakijitolea damu katika kituo cha Rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akikata utepe kuzindua kituo cha uchangiaji Damu salama cha Mbagala langitatu jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akizungumza leo katika uzinduzi wa Kituo cha Damu salama kilichopo Mbagara Rangitatu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki Baada ya kuzindua kituo cha uchangiaji Damu salama cha Mbagala langitatu jijini Dar es Salaam leo.
---

MPANGO wa Taifa wa damu salama nchini ulio chini ya wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto  leo wamezindua kituo kidogo cha uchangiaji damu kilichopo Mbagala Rangi tatu. Uzinduzi huu unaambatana na uzinduzi wa vituo vingine vya afya vilivyopo wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam kama vile Amana, Mwananyama, Sinza, Vijibweni na Mbweni.

Viituo hivi vimejengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ambao ni Hospitali ya CCBRT, Hospital ya Mbweni Mission MDH, Umoja wa wamiliki hospital binafsi (APHTA) NA Halmashauri za temeke Ilala na Kindondoni.  Vilevile  Mpango wa Taifa wa Damu salama unawapongeza wachangia damu kwa hiari ambao  wamekuwa wakichangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wahitaji tangu kampeni hii ilipoa nza rasmi tarehe 3 februari 2016.

Maisha ya watu wengi yanaokolewa kila mwaka nchini kwa kuongezewa damu . Nchini Tanzania kinamama wengi na watoto hupoteza maisha kwa kukosa damu. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha  kuwa nchini Tanzania takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000 hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya hivyo vifo husababishwa na ukosefu wa damu. Hivyo ufunguzi wa vituo hivi utasaidia kuondoa tatizo la uhaba wa damu na hatimaye kutokomeza tatizo la vifo vinavyotokana na kukosa damu.

Katika mkoa wa Dare s Salaam mahitaji ya damu ni makubwa , kwa mwezi tunahitaji chupa 4000 lakini zinazopatikana ni chupa 2000 tu ambayo ni nusu ya mahitaji. Kuna wakati mahitaji haya yanakuwa makubwa zaidi na hivyo upungufu huongezeka kufikia asilimia 70, hali ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.

Damu ni uhai na haipatikani kwa njia yeyote ile isipokuwa  kwa kuchangiwa na binadamu wenzetu . Uchangiaji damu ni zoezi endelevu na la kudumu kwakuwa damu huhifadhiwa kwa muda wa siku 35 tu tangu inatolewa . Kutokana na uhifadhi wa damu kuwa ni wa muda mfupi ndio maana inasisitizwa umuhimu wa watu kuchangia damu walau mara mbili kwa mwaka.
--

HOTUBA YA MHE SAID MECK SADIKI, MKUU WA MKOA WA
DAR-ES-SALAAM SIKU YA UFUNGUZI WA KITUO KIDOGO CHA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA MBAGALA
TAREHE 08 FEBRUARY 2016

·       Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya  ya Temeke
·       Mstahiki Meya wa Temeke
·       Mganga Mkuu Mkoa
·       Meneja wa Mpango wa Damu Salama Tanzania
·       Viongozi na Watendaji wa Serikali wote Mliopo Hapa
·       Wadau wetu wetu mlioshiriki katika uzinduzi wa leo
·       Ndugu  Wachangia Damu
·       Wanahabari
·       Wageni Waalikwa
·       Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote, namshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema na pia nawashukuru kwa kunialika kujumuika nanyi katika hafla  hii ya Uzinduzi wa vituo vya kuchangia damu hapa mkoani kwetu Dar-es-Salaam, vituo ambavyo vimejengwa kwa ushirikiano na wadau wetu kwa kushirikiana na Mkoa wetu wa Dar Es Salaam na Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Nawapongeza na kuwashukuru sana wadau wote ambao mmeshiriki kufanikisha zoezi hili.  Aidha niwapongeze sana wachangia damu wa hiari ambao wamekuwa wakichangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wahitaji tangu kampeni hii ilipo anza rasmi tarehe 03 february 2016

Ndugu Wananchi,
Maisha ya watu wengi yanaokolewa kila mwaka Nchini kwa kuongezewa damu, Nchini Tanzania kina Mama wengi na Watoto hupoteza Maisha kwa kukosa damu.  Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa nchini Tanzania takribani wanawake 432  kati ya vizazi hai 100,000 hufa kila mwaka kutokana na uzazi  na asilimia 80 ya hivyo vifo husababishwa na ukosefu wa damu hivyo ufunguzi wa vituo hivi kutasaidia kuondoa tatizo la uhaba wa damu na hatimaye kutokomeza tatizo la Vifo vinavyotokana na kukosa damuAlmost all of these deaths occur in developing countries. More than half of them occur in sub-Saharan Africa and almost one third in South Asia..

Katika Mkoa wetu wa Dar Es Salaam, mahitaji ya damu ni makubwa, kwa mwezi tunahitaji chupa 4,000 lakini zinazopatikana ni chupa 2,000 tu ambayo ni nusu ya mahitaji yetu.  Kuna wakati mahitaji haya yanakuwa makubwa zaidi na hivyo upungufu huongezeka kufikia asilimia 70, hali ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.

Ndugu Wananchi,
Jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa damu ya kutosha na iliyo salama, ni la wadau wote, i.e wananchi, viongozi wa idara za serikali, wanasiasa, na taasisi zisizo za serikari. Hivyo wote tujitambue  kuwa ni wadau wa Mpango wa Damu Salama, na hatuna budi kutoa ushirikianao pale wataalamu wa wafya  wafikapo katika maeneo yetu. Wote tukishirikiana tutaweza kufikia lengo la kupata damu ya kutosheleza mahitaji ya hospitali zetu na hivyo kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika.

Damu ni uhai na haipatikani kwa njia nyingine yeyote isipokuwa  kwa kuchangiwa na binadamu wenzetu. Uchangiaji damu ni zoezi endelevu na la kudumu kwa kuwa Damu huhifadhiwa kwa muda wa siku 35 tu tangu imetolewa. Kutokana na uhifadhi wa damu kuwa ni wa muda mfupi ndiyo maana inasisitizwa umuhimu wa watu kuchangia angalau mara mbili kwa mwaka. 

Ndugu Wananchi,
Kwa kuwa dhana ya kujitolea damu kwa hiyari bila malipo ni dhana mpya kwa walio wengi na imeripotiwa na Mpango wa damu salama kuwa moja ya changamoto ya upatikanaji wa Damu salama ni imani potofu na uelewa mdogo miongoni mwa wananchi, napenda nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi kwa  mambo yafuatayo:-

1)   Kwa nini inatubidi tuchangie damu?
Unapotoa damu, unachangia kuokoa maisha ya Mtanzania mwingine na hata ya ndugu yako wa karibu, zaidi ya 80% ya damu inayokusanywa hutumika kwa watoto chini ya miaka mitano, akina mama wenye matatizo ya ujauzito/uzazi na wahanga wa ajali.

2)   Je ni madhara gani yanatokea mtu unapojitolea damu?
Hakuna madhara yoyote yanayotokana na kuchangia damu. Mtu mzima ana wastani wa lita 5 za damu katika mwili wake. Kiasi kinachochukuliwa wakati wa kutoa damu ni 450ml, hii ni asilimia 10 tu ya damu yote mwilini. Baada ya kujitolea damu uwingi wa damu katika mwili hurudia hali ya kawaida ndani ya masaa 36.
3)   Je ni sifa gani au vigezo gani muhimu vya kuchangia damu?
•     Mtu yoyote mwenye afya njema,
•     Awe na uzito wa kuanzia 50kg ,
•     Umri wa kati ya miaka 18-65 na
•     Kwa wanawake, asiwe mjamzito au anayenyonyesha.
4) Ni mara ngapi mtu anaweza kuchangia damu/kujitolea damu?

 Aidha mtu anaweza kurudia kutoa damu kila baada ya miezi mitatu kwa wanaume na kila miezi minne kwa wanawake,.
 Mchangiaji anayeweza kujitolea damu angalao mara mbili kwa mwaka   anakuwa na sifa ya kuitwa mchangiaji damu wa kudumu.

Ndugu Wananchi,
Mpango wa Taifa wa Damu Salama unakabiliwa na changamoto ya kutofikia malengo ya ukusanyaji damu nchini.,tumesikia mahitaji ya damu kwa mwaka ni wastani wa chupa 400,000- 450,000 na ni Damu pekee ndio inayotumika kumuongezea mwenye kuhitaji kuongezewa damu, Mpango wa Taifa wa damu salama kutokukusanya damu ya kutosha kuna sababisha vifo vingi ambavyo vingeweza kuzuilika.  Hivyo katika kulitatua tatizo hili ni muhimu wananchi wajenge utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara
Ndugu  Wananchi,

Faida za kuchangia Damu kwa hiari ni kama zifuatazo;
-        Kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo: Kuwepo kwa madini chuma mengi kupita kiasi katika damu, hudhoofisha utendaji kazi wa baadhi ya kuta za moyo, kuchangia damu mara kwa mara, hurekebisha madini  chuma ya ziada  katika mfumo wa damu na kuondoa nishati joto isiyo ya lazima  kwenye damu ya mchangiaji kila baada ya kuchangia damu mililita 450. 

-        Upimaji wa Afya pasipo gharama: Kila wakati unapochangia damu, mtaalamu wa tiba, daktari au muuguzi atakupima shinikizo la damu, mapigo ya moyo na kukufanyia vipimo vingine vya magonjwa yaambukizwayo kwa damu bila malipo yeyote.
-        Huongeza utambuzi wa kiwango cha chembechembe za damu  katika mfumo wa uzalishaji  damu:
-        Seli za damu hupungua katika mzunguko wa damu yetu baada ya kuchangia,hivyo uchangiaji damu huchochea uzalishaji wa seli mpya za damu na kuchangamsha mfumo wa uzalishaji damu.

Ndugu Wananchi,
Leo nimeshiriki uzinduzi wa kituo kidogo cha kuchangia damu hapa Mbagala Rangi Tatu, huu ni mwendelezo wa juhudi za Mkoa wetu wa Dar Es salaam, Mpango wa Damu Salama na Wadau wetu   katika jitihada za  kusogeza huduma za kuchangia damu karibu na jamii. Kituo hiki na vingine vilivyopo hospital za Temeke, Mwananyamala, Amana, Sinza, Mnazi mmoja na Mbweni Mission   Mwanan hapa Dar-es-salaam vitatumika katika ukusanyaji na usambazaji damu kwa mkoa wa Dar-es-salaam, Ni matumaini yangu wakazi wa Dar-es-saam mtahamasika kuendelea kuchangia damu na hatimaye mkoa wetu uondokane na tatizo la ukosefu wa  damu salama
Ndugu  Wananchi,
Niruhusuni nimalize hotuba yangu kwa kushukuru Wizara yetu ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Timu ya kuratibu huduma za Afya Mkoa, Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Halmashauri zetu za Temeke, Ilala na Kinondoni, Hospitali ya CCBRT, Hospitali ya Mbweni Mission MDH, Umoja wa wamiliki wa Hospitali binafsi (APHTA), na kamati ya maandalizi kwa kufanikisha uzinduzi huu ambao umefana sana. Pia napenda kutoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari ili Taifa liwe na akiba ya damu ya kutosha na hatimaye kupunguza vifo ambavyo vinaweza sababishwa na ukosefu wa damu
Sasa nichukue fursa hii kutamka kwamba Kituo Kidogo cha kuchangia Damu Mbagala Rangi tatu , (Satellite Blood Centre) kimezinduliwa rasmi.  

KWA PAMOJA TUSEME KAULI MBIU YETU
“CHANGIA DAMU OKOA MAISHA”

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: KIDOGO CHA UCHANGIAJI DAMU CHA MBAGALA RANGI TATU JIJINI DAR CHAZINDULIWA LEO.
KIDOGO CHA UCHANGIAJI DAMU CHA MBAGALA RANGI TATU JIJINI DAR CHAZINDULIWA LEO.
https://3.bp.blogspot.com/-Q-NmBlg1nhs/VritL4-i27I/AAAAAAADeu4/akk19rJvSQA/s640/DSC_0377%2B-%2BCopy.JPG
https://3.bp.blogspot.com/-Q-NmBlg1nhs/VritL4-i27I/AAAAAAADeu4/akk19rJvSQA/s72-c/DSC_0377%2B-%2BCopy.JPG
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/02/kidogo-cha-uchangiaji-damu-cha-mbagala.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/02/kidogo-cha-uchangiaji-damu-cha-mbagala.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago