Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA PROFESA SOSPETER MUHONGO AKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA NISHATI LENGO KUZALISHA MEGAWATI 10,000 IFIKAPO MWAKA 2025 JANUARI 05, 2016

  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akielezea mikakati na fursa zilizopo katika sekta ya nishati.   Mkurugenz...

 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akielezea mikakati na fursa zilizopo katika sekta ya nishati.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtibwa Sugar Estates Ltd, Nassor Seif akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni ya Mtibwa Sugar Estate Ltd.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na kampuni ya Mtibwa Sugar Estates Ltd.   Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo  kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme ili kukidhi mahitaji yake zaidi.
--
Na Greyson Mwase, Dar es salaam
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka wawekezaji  kutoka ndani na nje ya nchi  kujitokeza zaidi ili kuwekeza kwenye  uzalishaji wa umeme  nchini lengo likiwa ni kufikisha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake kilichoshirikisha watendaji wa  wizara  ya nishati na madini na kampuni ya  kuzalisha sukari ya  Mtibwa Sugar  Estates Limited.
Alisema kuwa  lengo la serikali ni kuhakikisha  sekta ya  nishati inachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi  kupitia uzalishaji wa umeme wa uhakika utakaopelekea ongezeko la  viwanda nchini.
Aliongeza kuwa  ili nchi  yoyote duniani iweze kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi wake, inahitaji umeme wa uhakika na kusisitiza kuwa serikali inabuni vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha  kuwa umeme wa uhakika unapatikana.
Aliendelea kusema kuwa ongezeko la  viwanda litapekelea ajira kuongezeka na uchumi  kukua kuanzia  ngazi  ya wilaya hadi  nchi kwa ujumla.
Profesa  Muhongo  aliitaka kampuni ya  Mtibwa Sugar Estates Ltd kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme zaidi na kuliuzia  Shirika la  Tanesco ili kupunguza tatizo la mgawo wa umeme nchini.
Akielezea mikakati ya serikali katika  uimarishaji wa sekta ya  umeme nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa kupitia Wakala wa Nishati  Vijijini (REA)  serikali imekuwa ikiwaunganishia wananchi waishio  vijijini  umeme kupitia awamu tofauti tofauti.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA PROFESA SOSPETER MUHONGO AKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA NISHATI LENGO KUZALISHA MEGAWATI 10,000 IFIKAPO MWAKA 2025 JANUARI 05, 2016
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA PROFESA SOSPETER MUHONGO AKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA NISHATI LENGO KUZALISHA MEGAWATI 10,000 IFIKAPO MWAKA 2025 JANUARI 05, 2016
http://4.bp.blogspot.com/-anyKre4nr8E/VoviWzBxvbI/AAAAAAADdSg/nG4luPuESK8/s640/mt2.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-anyKre4nr8E/VoviWzBxvbI/AAAAAAADdSg/nG4luPuESK8/s72-c/mt2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/waziri-wa-nishati-na-madini-profesa.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/waziri-wa-nishati-na-madini-profesa.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago