Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga,akutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba, akisalimiana na Mh. Shy-Ros...

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba, akisalimiana na Mh. Shy-Rose Bhanji
 Dkt. Mahiga, akisaliamiana na mmoja wa wabunge hao, Mh. Shy-Rose Bhanji
  Mh. Shy-Rose Bhanji akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (wakwanza kushoto) na maafisa wengine wa wizara hiyo, mara baada ya kikao hicho
 Mh. Makongoro Nyerere, akipena mikono na Bi. Mindi Kasiga
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao walikwenda kumsalimia waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
---
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15, 2016 amekutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania waliokwenda kujitambulisha na kubadilishana mawazo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 
Wabunge hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard Murunya.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho kifupi cha kutambuana.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika kujitambulisha kwa Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara hiyo, tulikuwana Dkt. Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa hivyo tuliona ni vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” AlisemaMh. Makongoro na kuongeza, “Lakini pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA, vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh. Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo sio busara tukakutanie kule ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa atutambue na kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh. Makongoro.

Bunge la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya Afrika Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambaonipamoja na Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga,akutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga,akutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania
http://4.bp.blogspot.com/--kwDyw3540w/VpjxEpXn-eI/AAAAAAADdqQ/ZiFamLxYhzI/s1600/Shy_Naibu%2Bwaziri.jpg
http://4.bp.blogspot.com/--kwDyw3540w/VpjxEpXn-eI/AAAAAAADdqQ/ZiFamLxYhzI/s72-c/Shy_Naibu%2Bwaziri.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/waziri-wa-mambo-ya-nje-na-ushirikiano.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/waziri-wa-mambo-ya-nje-na-ushirikiano.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago