Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI- MHE. JORGW LUIS LOPEZ TORMO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo,  ofisini kwake jijini Dar es slaam Jan...

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo,  ofisini kwake jijini Dar es slaam Januari 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo, kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es slaam Januari 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
---
 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Bwana Jorge Luis Lopez Tormo ambaye ameahidi kuendelea kusaidia Tanzania katika mapambano dhidi ya malaria.

Akizungumza na Balozi  Tormo leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo, kwa Serikali ya Cuba kuendelea kusaidia Tanzania katika mapambano  dhidi malaria  kwa kusaidia ujenzi wa kiwanda cha  kwanza Afrika cha  viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria kilichopo, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani  kinachosimamamiwa na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).

 “Nawashukuru sana kwa namna mnavyosaidia kupambana na malaria, kupitia mradi huo mkubwa Afrika ambao unalenga kumaliza ugonjwa wa malaria,unaosababisha idadi kubwa ya vifo katika nchi yetu.” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Pia, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha  raia wa Cuba kuja kuwekeza nchini hasa   katika teknolojia. Na ameahidi kuendeleza uhusiano mwema ulipo baina ya nchi hizi mbili.

Waziri  Mkuu ameendelea kwa kusema kuwa Cuba ni nchi  iliyoendelea katika biashara, viwanda na uwekezaji  na imefanikiwa  kutoa bure huduma za kijamii ikiwemo afya, hivyo Serikali ya Tanzania haina budi kujifunza kutoka kwao ili kutimiza azma yake ya kutoa bure huduma mbalimbali za kijamii kama ambavyo sasa  inatolewa elimu bure.

 Kwa upande wake, Balozi Tormo   amesema kuwa pamoja na Serikali ya Cuba kusaidia kutoa wataalamu katika kujenga kiwanda hicho cha   viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria ambao utanufaisha pia nchi za jirani siku za usoni, wanapenda kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika kuzalisha wataalamu kupitia programu mbalimbali ikiwemo afya na elimu. Mfano progamu inayoendelea ya kubadilishana  wataalamu katika kitivo cha madawa cha Chuo Kikuu Cha Zanzibari (SUZA).

“Tunaweza kuendeleza program za kujifunza lugha ya Kiswahili, kama hapo awali, hii ni njia nzuri na muhimu ya kuendeleza uhusiano wetu na watu kuelewa lugha zetu”, alisema Balozi Tormo.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI- MHE. JORGW LUIS LOPEZ TORMO
WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI- MHE. JORGW LUIS LOPEZ TORMO
http://4.bp.blogspot.com/-cPoBiNGodQg/VpOpMK_0ASI/AAAAAAADdhM/Nlyg9jW78sc/s640/MAJ2.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-cPoBiNGodQg/VpOpMK_0ASI/AAAAAAADdhM/Nlyg9jW78sc/s72-c/MAJ2.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/waziri-mkuu-kassimu-majaliwa-akutana-na.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/waziri-mkuu-kassimu-majaliwa-akutana-na.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago