Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

UZINDUZI WA STIKA MAALUM YENYE UJUMBE WA KUTOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

 Na Nyakongo Manyama-MAELEZO TAASISI ya  watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa  ‘stika’ ...

 Na Nyakongo Manyama-MAELEZO
TAASISI ya  watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa  ‘stika’ maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye albinism utakaofanyika januari 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. Michael Lugendo amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika kituo cha polisi kati jijini Dar es Salaam kuanzia saa tano asubuhi.

Bw. Michael Lugendo amesema kuwa stika hiyo ina lengo la kuhamasisha jamii kuungana na Rais Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam ili kuyafanya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yatokomezwe na yabaki kuwa historia.

Kwa upande mwingine Bw. Lugendo ameongeza kuwa kulingana na kasi ya mabadiliko tabia nchi, jamii isipochukua hatua za makusudi kuna uwezekano wa watu wenye ulemavu wa ngozi kuangamizwa na saratani ya ngozi.

Alisema watu wenye ulemavu wa ngozi wanaishi katika mazingira ya umaskini kiasi kwamba waliowengi hawana uwezo wa kupata fedha ya kununua mafuta ya kuzuia mionzi ya jua  ambayo husababisha saratani ya ngozi.

“Sisi watu wenye ulemavu wa ngozi ni wahanga wakubwa sana na jamii isipochukua hatua za makusudi upo uwezekano wa kuangamizwa na saratani ya ngozi ukizingatia kwamba tunaishi katika mazingira ya umaskini na walio wengi hatuna uwezo wa kupata fedha ya kununua mafuta” alisema Bw. Lugendo.

Aidha Bw. Lugendo amesema kuwa  taasisi hiyo imemteua Bw. Mbwana Ally Samata kuwa balozi wa kudumu wa kusemea watu wenye ulemavu wa ngozi.

Alibainisha kuwa majukumu ya Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Tanzania kwa ujumla ni kuhamasisha dunia kwa njia ya soka kuhakikisha  kwamba hakuna mlemavu wa ngozi anayefariki kwa kifo cha saratani ya ngozi au mauaji ya kukatwa viungo yanayotokana na Imani za kishirikina.

Bw. Lugendo aliwataka wadau mbalimbali, kampuni, balozi mbalimbali, Mashirika yasiyokuwa ya Serikali kujitokeza ili kuwezesha kutimiza lengo hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kupitia vyombo vya habari pamoja na jeshi la polisi.

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: UZINDUZI WA STIKA MAALUM YENYE UJUMBE WA KUTOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO
UZINDUZI WA STIKA MAALUM YENYE UJUMBE WA KUTOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO
http://1.bp.blogspot.com/-AFO3td5oBXM/Vpj7wVCUmLI/AAAAAAADdrg/Je6YMR2nC60/s640/LUG.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-AFO3td5oBXM/Vpj7wVCUmLI/AAAAAAADdrg/Je6YMR2nC60/s72-c/LUG.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/uzinduzi-wa-stika-maalum-yenye-ujumbe.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/uzinduzi-wa-stika-maalum-yenye-ujumbe.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago