Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TAMKO LA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA)

TAMKOLA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA) KUHUSUMAELEZO YA WAZIRI WA AFYA ALIYOYATOA TAREHE 15/01/2016, JUU ...

TAMKOLA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA
(SHIVYATIATA)

KUHUSUMAELEZO YA WAZIRI WA AFYA ALIYOYATOA TAREHE 15/01/2016, JUU YA TIBA ASILI NATIBA MBADALA.

Ndugu waandishi wa Habari na ndugu wananchi,shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania (shivyatiata) ni chombokinachosimamia vyama vyote vya Tiba Asili hapa Nchini pamoja na Waganga wote waTiba Asili na pia ndiyo msemaji wao kwa Serikali, Mashirika ya Kitaifa naKimataifa na kuhakikisha chombo hiki kinasimamia na kulinda maslahi yote yaWaganga wa Tiba Asili hapa nchini
Hivyo basi ,kutokana na maelezoyaliyotolewa na Waziri mwenye dhamana na mambo ya Afya mnamo hiyo tarehe15/01/2016 shirikisho kwa kutambua dhamana tuliyonayo mbele ya Umma wa Wagangatunapenda kuwasilisha tamko letu kwenu nyinyi waandishi wa Habari na wanchi kwaujumla ili muweze kuelewa yanayoendelea katika Tiba Asili hapa nchini.
Ndugu waandishi wa Habari, kwanzamtakumbuka kuwa mnamo tarehe 14/12/2015 Naibu waziri wa Afya maendeleo yaJamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Dkt HAMISI KIGWANGALA (MB) alifanya ziarakatika kituo cha Tiba Mbadala cha Tabibu anayejulikana kwa jina la Dr MWAKA.Baada ya ziara hiyo mengi yalizungumzwa na hata tamko la Wizara lililotolewaterehe 24/12/2015 lililohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa upande mmoja nalolilichangia kuwepo kwa malumbano ya hapa na pale kutoka kwa watoa huduma waTiba Asili na Tiba Mbadala, na wengine wakafikia  hatua ya kupinga  agizo hilo na kuitisha mgomo.
Ndugu waandishi wa Habari tunapendamfahamu kuwa Wizara ya Afya katika kufikia kutoa tamko  hilo la tarehe24/12/2015 hawakushirikisha chombo chenye dhamana ya waganga ambacho nishirikisho hili la vyama vya Tiba Asili Tanzania, Lakini kwa kutambua dhamanatuliyonayo kwa waganga wote wa Tiba Asili na kwa kutambua kuwa popotepanapokuwa na mgogoro basi njia sahihi ni kukaa mezani kujadiliana ili hatimaye amani ipatikane.
Hivyo sisi Shirikisho tuliomba kikaona Mh. Waziri wa Afya ambacho kilifanyika tarehe 28/12/2015 na ambachokilionesha nuru ya kufikia maelewano, Na kwa kuwa siku hiyo  tarehe 28/12/2015 Waziri wa Afya Mhe. UMMYMWALIMU alitamka mbele ya vyombo vya habari kuwa yupo tayari kukaa kujadilianana yeyote Yule ambaye amekwazwa na agizo la Wizara.
Hivyo sisi shirikisho tuliweza kukaana wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ambao kimsingi ndiyo haswa walikwazikana agizo hilo la Wizara na hatimaye tarehe 31/12/2015 tulifanya kikao chapamoja kati ya wadau hao, shirikisho, na Wizara ya Afya tukiongozwa naUenyekiti wa  Mhe. UMMY MWALIMU (MB) ambayendiye waziri mwenye dhamana na mambo ya Afya .
Ndugu waandishi wa Habari napendaifahamike kuwa kikao hicho cha tarehe 31/12/2015 tulikubaliana kuwa wale wotewanaopeleka matangazo yao na vipindi kwenye Baraza kwa ajili ya kuhakikiwa basiBaraza liwaruhusu kuendelea na program yao hiyo na uhakiki wa Baraza usizidisiku tatu (3) kwa ujumla makubaliano yote ilikuwa ni utekelezaji wa sheria  namba 23 ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 na kanuni zake na pia sherianyinginezo za nchi na pia utekelezaji huu uwe wa pande zote, na mwisho Mhe Wazirialituhaidi kuwa tamko lingine la Serikali litatolewa  tukiwa wote.
Lakini katika  hali ya kushitua na kushangaza Mhe Waziri waAfya ametoa tamko bila ya kutushirikisha sisi wadau wengine kama tulIvyokubaliana.
Hivyo tunaamini Waziri asingefanyahivyo kukiuka makubaliano isipokuwa ni kushauriwa vibaya na vyombo vya chiniyake ambavyo vinadhammana ya kumshauri juu ya Tiba na tunaamini hivyo kwa kuwaviongozi wenye dhamana ya kumshauri walio chini yake wao ni wanataaluma yaUdaktari wa kisasA, Hivyo wameshindwa kumshauri Waziri vizuri kwa  sababu wanapigania maslahi ya Taaluma yaonahawapo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tiba Asili, lakini tunamuomba Mhe.Waziri kwa kuwa yeye ni mwanasheria basi aimome sheria namba  23 vizuri ili aweze kujiridhisha.
Tunaamini kuwa viongozi hao waliochini yake wangetumia nafasi na dhamana waliyo nayo kumshauri Mhe Waziri vizurijuu ya Tiba Asili  bila kuweka mbelemaslahi ya Taaluma yao, basi yote haya yasingetokea .
Ndugu waandishi wa Habari, Tiba Asiliimekuwepo hapa nchini kwa mika mingi kabla ya kuja  tiba ya Kisasa ambayo kwa kadri sikuzinavyozidi  nayo inazidi kupotezaumaarufu wake na kuiacha Tiba Asili ikizidi kuchukua nafasi kubwa katika nchiyetu, Hivyo kitendo cha Tiba Asili na Sasa Tiba Mbadala  kuzidi kuchukua nafasi kubwa  kwa wananchi ambayo hivi sasa ni asilimia 70%mijini na asilimia 80% vijijini wanatumia Tiba Asili kitendo hicho kinawakerahao wanaoitwa madaktari wa kisasa na ndiyo maana maneno yamekuwa mengi kwaupande huu waTiba Asili na Tiba mbadala na kufikia hata hatua ya kutukejeri etikwa nini tunavaa mavazi  meupe wakati wakutoa tiba?, kwa nini tunaitwa  Madaktarikama wao? Na wengine hufikia kusema eti sisi waganga wa Tiba Asili na Tibambadala unaongoza kusababisha Vifo vya Wagonjwa kitu ambacho siyo kweli hatakidogo kwani Tiba Asili imeokoa na inazidi kuokoa maisha ya watu wengi mijinina vijijini, mfano mdogo katika Tiba Asili yapo magonjwa mengi yasiyoambukizatunayatibu na pia tunaunga mifupa na waliovunjika hurejea katika hali yao yakawaida ndani ya wiki mbili hadi mwezi mmoja kitu ambacho kwa Tiba ya Kisasaimekuwa ndoto kwao,
Lakini vilevile Tiba hiyo ya Kisasandiyo inaongoza kwa vifo vya watu wengi mijini na vijijini na ushaidi wa hiloni uwepo wa  mochwari karibu kilahospitali kwa ajili ya kuhifadhia maiti zitokanazo na watu waliokuwa niwagonjwa na wakitibiwa katika Hospitali hizo na hao Madaktari bingwa wa Kisasa.
Ndugu waandishi wa Habari na nduguwananchi, shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania tunapinga vikali matamshiyote yanayotolewa yakiwa yanalenga kuidhalilisha Tiba  yetu ya Asili ambayo imekuwepo hapa nchinikwa miaka mingi na kwa sasa tunaiboresha na kuiendeleza ili iwe ya kisasazaidi.
Hatupo tayari kuona watoa  huduma wa Tiba Asili wananyanyaswa nakudhalilishwa ndani ya nchi yao, Hii ni nchi yetu sote.
Hivyo hakuna mwenye haki ya kujionakuwa yeye na kundi lake ndiyo  bora nawengine siyo bora,  yeye ndiyo anahaki yakuzungumzia mwili wa mtu na wengine hawana haki hiyo, yeye ndiyo ana haki yakuvaa koti jeupe wakati wa kutoa Tiba na wengine haki yao ni kuvaa kaniki.
Kama kuna watu wapo tayari kuona hayoyanaendelea kutendeka  sisi tunasemahatuko tayari na muda wote hatutokuwa tayari.
Hivyo katika hili  tamko lililotolewa tarehe 15/01/2016 na MheWaziri wa Afya tunabainisha mambo gani tunayaunga mkono na mambo ganihatuyaungi mkono
MAMBO TUNAYOYAUNGA MKONO
1.   Tunaungamkono Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuongezwa watumishi wa kutosha lakini wawe na moyo wa  kuipenda Tiba Asili na Tiba mbadala
2.   Tunaungamkono kuwepo mpango mkakati kwa muda mrefu kuwezesha kufanikishauboreshaji  wa Huduma wa Tiba Asili naTiba mbadala lakini mpango huo uwe wa vitendo zaidi.
3.   Tunaungamkono watoa huduma wote, vituo vyote vya kutolea huduma, dawa na vifaa tibavinasajiliwa .
4.   Tunaungamkono mwongozo wa  mafunzo kwa watoahuduma  wote  nchini kuhusu namna ya kuweka  kumbukumbu za wagonjwa , kutoa rufaa kwawagonjwa (lakini rufaa hizo ziwe kwa pande zote siyo waganga tu kupelekawagonjwa mahospitalini na mahospitali nayo yalete wagonjwa wao kwa waganga waTiba Asili na Tiba Mbadala)
5.   Piatunaunga mkono kuwepo kwa mawasiliano kati ya Wizara Afya na Wizarazinazohusika na mambo ya Habari, OFISI YA RAIS Tamisemi, na Taasisi za utafiti
MAMBO AMBAYO HATUYAUNGI MKONO
1.   Hatuungimkono kuondolewa kanuni  inayoruhusumatangazo kwa idhini ya Baraza isipokuwa tunataka sheria iachwe kama ilivyo juu ya utoaji wa matangazo .
2.   Hatuungimkono kuongezwa adhabu kwa sababu hata iliyopo haijawahi kutumika kwa wakosaji
3.   Hatuungimkono kuweka ukomo wa usajili mijini  navijiji kwa sababu tangu usajili uzinduliwe ni miaka mitano sasa na wagangawaliosajiliwa hawazidi elfu kumi na moja (11,000), Hivyo siyo kazi rahisikusajili waganga elfu sitini na nne(64,000) kwa muda wa miezi mitatu na sita,ikiwa wapo watu  wamejaza fomu za Barazatangu mwaka 2011 na walilipia  Ada  za usajili Banki lakini hadi leo hawajapata vyeti, kwa hiyo hata hatua yakuwazuia wasitoe huduma hilo haliwezekani.
4.   Hatuungimkono kuzuia kuuza dawa au kugawa dawa eti hadi iwe imesajiliwa na Baraza,kupimwa na maabara ya mkemia mkuu wa serikali na kupewa kibali na TFDA hilohalikubaliki kwa sababu tunaamini kuwa TFDA ni mmoja ya wanaosababisha migogoroya Waganga ikiwemo kutoa vibali vya waganga kutangaza katika Radio na Televisheni  na hali hawaruhusiwi kutoa vibali hivyolakini Wizara ya Afya wameshindwa kuikemea TFDA, Tunataka utaratibu wa kupimadawa, kusajili katika Baraza uende sambamba na uuzaji na ugawaji wa dawa hizokwa wagonjwa .
5.   Hatuungimkono  agizo la kusajili vifaa tiba TFDAkwani agizo hilo siyo la kisayansi na halitekelezeki kwa mazingira yaliyopohapa nchini ambayo hivi sasa wapo watu wengi wananunua na kutumia vifaa tibakwa ajili ya kujiangalia Afya zao kwa hiyo siyo kazi rahisi kwa mtu binafsikwenda kusajili mashine ya Glukosi TFDA tunataka waachwe wavitumie kwa kuwa waondiyo wanavitumia na kuviamini.
6.   Hatuungimkono kuzuia matangazo ya aina yoyote yanayohusu Tiba Asili kwa sababu sheriainaelezea utaratibu wa kutangaza , na pia tunaomba ifahamike kuwa matangazoyanayohusu Tiba Asili hayamuthiri mwananchi yeyote ikilinganishwa matangazo yasigara na vilevi vingine lakini Wizara ya Afya ipo kimya juu ya matangazo hayona kuacha watu wengi wakiangamia kwa kutumia vitu hivyo. Kama hoja ni Tibaisitangazwe kwa Dunia ya sasa haiwezekani watu ni wengi na vifaa vya kutangaziavipo, zamani watu walikuwa wachache  nahakukuwa na vifaa vya kutangazia, isitoshe hata Ibada zinatangazwa kwanza ndiyoutaona watu wanajaa makanisani na misikitini kwa hiyo kusema Tiba isitangazwehaikubaliki hata kidogojambo la msingi ni kuboresha utaratibu iliopo unaohusumatangazo na siyo kuuondoa .
Uganga wa Tiba Asili naTiba Mbadala siyo jambo la kuhujumu uchumi wala madawa ya Tiba Asili si madawaya kulevya . Na pia kuwazuia watoa huduma kutoa elimu kwa umma kupitia vyombovya habari na mikutano ya hadhara kuhusu Tiba Asili na Tiba Mbadala nalohalikubaliki  hata kidogo, Huo ni uvunjifuwa katiba na ni kinyume cha haki za Binadamu na pia  itakuwa ni kuingilia Taaluma ya Mtu,isipokuwa zuio liwe kwa  mtu ambaye siMganga.
Hivyo basi kutokana nahayo tuliyoyaeleza  tunaamini kuwa sisiwaganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala tunahujumiwa na tunaamini kabisa wapowatu hawaitakii mema tiba yetu hii, hivyo tunataka mambo yafuatayoyatekelezwe:-
1.   Viongoziwote wenye dhamana ya kumshauri Waziri juu ya Tiba kwa kuwa wameshindwakumshauri vema na wameegeme kupendelea Taaluma yaoTunaomba mamlaka ya juuiingilie swala hili ili  haki itendeke
2.    Tiba Asili iundiwe Wizara yake kwa sababumadaktari wa kisasa sisi tunawapenda lakini wao hawatupendi  wanaonaWizara ya Afya ni ya kwao peke yao.
3.   Ilituwe na Imani na Wizara ya Afya tunataka tuwe na Mganga mkuu wetu wa Tiba Asilina Tiba Mbadala wa serikali kuliko kuwa na hawa wa kawaida ambao kazi yao kubwani  kupendelea Taaluma zao.
4.   Kuanziasasa Waganga wote wasajiliwe na shirikisho kwa kuwa ndiyo linaweza kuwatambuana kuwafuatilia kwa karibu utoaji wao wa huduma na Baraza libaki na kazi yakuthibitisha vyeti vyao tu .
5.   Tunatakaheshima ya Tiba Asili ienziwe na siyo kudharauliwa.
6.   Tunatakawaziri mwenye dhamana na Afya awaeleze Watanzania ni watu wangapi wanakufa  kwa siku katika hospitali za serikali na zaBinafsi ambazo zina hao wanaoitwa Madaktari bingwa.
7.   Mamlakaya juu ya Wizara ya Afya kwa maana ya Ofisi ya Waziri mkuu tunaomba iingiliekati swala hili, ikae na sisi wadau wa Tiba Asili ili ukweli ujulikane namuafaka upatikane  tunaamini katikamajadiliano, na tunaimani na Serikali yetu inayoongozwa na Mhe.Rais  Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI.

 Ahsanteni sana kwakunisikiliza


ABDULRAHMANM. LUTENGA
Mwenyekitiwa Taifa wa Shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania

Tarehe16/01/2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TAMKO LA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA)
TAMKO LA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA)
http://1.bp.blogspot.com/-J25ES5Xfv_E/Vp9HVCsm6pI/AAAAAAAA5dU/vx1UrSUlL9o/s320/image.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-J25ES5Xfv_E/Vp9HVCsm6pI/AAAAAAAA5dU/vx1UrSUlL9o/s72-c/image.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/tamko-la-shirikisho-la-vyama-vya-tiba.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/tamko-la-shirikisho-la-vyama-vya-tiba.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago