Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TAARIFA KWA UMMA:WAZIRI OFISI YA RAIS-TAMISEMI GEORGE SIMBACHAWENE AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA KIGOMA NA MPANDA MKOANI KATAVI KWA KUSABABISHA UPOTEVU WA FEDHA ZA SERIKALI

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene -- JAMHURI YA MUUNGANO WA ...

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene (Mb) amewasimamisha kazi Wakurugenzi Watendaji wa Manispaa za Kigoma, Mkoa wa Kigoma na Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuridhia na kutekeleza maamuzi ambayo yamesababishia Serikali hasara na upotevu wa fedha.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Mhandisi Boniface Nyambele anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na bila kibali cha Waziri Mwenye Dhamana kama Sheria inavyo elekeza.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Ndugu Suleiman Lukanga ana kabiliwa na tuhuma za Ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi cha shilingi milioni tisini na mbili na laki saba na elfu hamsini (92,750,000/=) na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kakese kiasi cha shilingi milioni mia mbili, tisini na nne (294,000,000/=).

Aidha, Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari Ndilowa ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Ndugu Lauteri John Kanoni ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, amewataka  Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate  Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.  Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Tarehe 18 Januari, 2016

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TAARIFA KWA UMMA:WAZIRI OFISI YA RAIS-TAMISEMI GEORGE SIMBACHAWENE AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA KIGOMA NA MPANDA MKOANI KATAVI KWA KUSABABISHA UPOTEVU WA FEDHA ZA SERIKALI
TAARIFA KWA UMMA:WAZIRI OFISI YA RAIS-TAMISEMI GEORGE SIMBACHAWENE AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA KIGOMA NA MPANDA MKOANI KATAVI KWA KUSABABISHA UPOTEVU WA FEDHA ZA SERIKALI
http://2.bp.blogspot.com/-hgXzTmsABfM/VpzxruWQ2qI/AAAAAAADdto/-x3d2iPopck/s640/simbaa.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-hgXzTmsABfM/VpzxruWQ2qI/AAAAAAADdto/-x3d2iPopck/s72-c/simbaa.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-ummawaziri-ofisi-ya-rais.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-ummawaziri-ofisi-ya-rais.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago