Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

TAARIFA KWA UMMA:HATUA KALI ZITACHUKULIWE KWA WANAOOZA WATOTO

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZAZI NA WATOTO  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi...

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZAZI NA WATOTO
 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa masikitiko makubwa na inataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wazazi wawili tofauti wanaotuhumiwa kuwaozesha watoto wao wa umri wa miaka 13 na kuwakatisha masomo katika mkoa wa Shinyanga na Dodoma Imeelezwa kuwa, wakati mtoto mmoja mwanafunzi wa shule ya msingi Wishiteleja wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga ameozeshwa kwa nguvu kwa mahari ya ngombe 13 na kumkatisha masomo yake akiwa darasa la sita, mtoto mwingine wa mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato Manispaa ya Dodoma anasemekana kuozeshwa kwa mahali ya shilingi 600,000. Kufuatia kuwepo kwa matukio haya mawili Wizara inataka vyombo vya dola kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi wa Mtoto katika mikoa yote kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanachukuliwa hatua kali. 

Tukio la kuwaoza watoto katika umri mdogo siyo tu linakinzana na haki za msingi za mtoto bali pia linamkosesha mtoto haki ya kuendelezwa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha uhai wake kwa kupatiwa majukumu ya mtu mzima katika umri mdogo.  

Wizara inawataka wazazi na walezi kubadilika na kuachana na tabia ya kuwaoza watoto wao katika umri mdogo maana vitendo hivyo ni vya kikatili. Jamii inatakiwa kutambua kuwa, vitendo  vya kikatili kama hivyo vinapofanywa katika familia vinarudisha nyuma juhudi za Serikali za kupambana na ukatili maana kwa kiasi kikubwa familia inatakiwa kuwa mahala salama panapofaa watoto kuishi na kulindwa.

Aidha, Wizara  inakumbusha wazazi, walezi na wadau wengine kuwa, ndoa za utotoni ni kinyume na Sheria ya Mtoto (2009) na Mikataba ya Kimataifa kuhusu Haki na Ustawi wa Mtoto. NIwajibu wa kila mtu kuhakikisha kuwa watoto wanaishi katika usalama na  kuhakikishiwa  haki zao zote  za msingi ikiwemo kulindwa, kuendelezwa, kuishi  na kushirikishwa katika maisha ya kila siku ili kujenga Taifa linaloheshimu maslahi ya watoto.

Erasto T. Ching’o
 Kny:    KATIBU MKUU
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZAZI NA WATOTO

COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: TAARIFA KWA UMMA:HATUA KALI ZITACHUKULIWE KWA WANAOOZA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA:HATUA KALI ZITACHUKULIWE KWA WANAOOZA WATOTO
http://1.bp.blogspot.com/-PWhiejt-m0w/VpePALubV1I/AAAAAAADdos/MdoW3L9tj54/s200/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
http://1.bp.blogspot.com/-PWhiejt-m0w/VpePALubV1I/AAAAAAADdos/MdoW3L9tj54/s72-c/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-ummahatua-kali.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-ummahatua-kali.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago