Archive Pages Design$type=blogging

How to make a Website

Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara yaNchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira:Serikali kuimarisha NEMC, yasimamisha maafisa wake kadhaa na wengine wapewa onyo

January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ---  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI Y...


January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
--- 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA  RAIS

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

Katika kikao kilichoitishwa na Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tarehe 24 January 2016, kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

a. Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,

b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II

c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira

Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia

2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kalian la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.

3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwenye Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

IMETOLEWA NA

IDARA YA MAZINGIRA,

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

TAREHE 24.01.2016COMMENTS

Name

9 Habari hii na Leila Abdul Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni leo mjini Dodoma.Na Msimbe Lukwangule Mahafali Picha na Mdau Abdallah Mrisho Salawi tangazo Uchambuzi huu kwa Msaada wa Dr Faustine Update kutoka Dodoma na Msimbe Lukwangule zilipendwa
false
ltr
item
H@ki Ngowi: Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara yaNchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira:Serikali kuimarisha NEMC, yasimamisha maafisa wake kadhaa na wengine wapewa onyo
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara yaNchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira:Serikali kuimarisha NEMC, yasimamisha maafisa wake kadhaa na wengine wapewa onyo
http://4.bp.blogspot.com/-9T5MIQls0R4/VqY8DSD3j4I/AAAAAAADeIc/aBb9V78mWTE/s640/EDWI6315.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-9T5MIQls0R4/VqY8DSD3j4I/AAAAAAADeIc/aBb9V78mWTE/s72-c/EDWI6315.jpg
H@ki Ngowi
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-umma-kutoka-wizara-yanchi.html
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/
http://www.hakingowi.com/2016/01/taarifa-kwa-umma-kutoka-wizara-yanchi.html
true
5996140674267894691
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago